Jumatano, 20 Desemba 2017
Jumatatu, 18 Desemba 2017
Jumapili, 17 Desemba 2017
Msigwa chomeni nyumba Moto Kama nitahamia CCM
Mbunge
 wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini 
kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama 
cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.
Msigwa
 amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa 
wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa 
na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni 
kuuza hadi utu wa wapiga kura.
Msigwa
 ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa 
chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila 
hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.
"Nikihamia
 CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu  na magari yangu. Sikuingia
 bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna 
agenda na kozi kama chama tunapigania.  Mkome kabisa kunipigia simu mimi
 sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa
Akizungumzia
 kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa 
kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni 
kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM 
nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi 
wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I 
am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi
Aidha
 Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa 
kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni 
na kuongeza kwamba  alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na 
mbunge.
"Sikuingia
 Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu 
wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa 
wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi 
wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta 
bungeni.  Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi 
ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.
Jumanne, 21 Novemba 2017
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)


















































