Ijumaa, 3 Februari 2017
Wasanii watii Amri ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda
TID akiingia lango la central polisi
Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwataka baadhi ya mastaa wanaoshukiwa kujihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuwasili kituo cha polisi cha kati siku ya leo baadhi ya mastaa wametii agizo hilo na kuwasili.
Wema Sepetu ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Da es salaam Paul Makonda kwamba anatumia Madawa ya kulevya, amewasili kituoni hapo huku akiwa amevalia vazi la hijab.
Wasanii wengine waliofika kituoni hapo ni pamoja na TID, Nyandu Tozzy pamoja na mtangazaji wa Clouds TV Babu wa Kitaa.
#MAGAZETINI LEO# Rais Magufuli aitaka Mahakama kufuatilia madeni ya kesi serikali ilizoshinda
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito
kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya
serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana
jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka
mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati
kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Alisema
kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za
kodi ambapo Serikali imeshinda kesi hizo japo fedha hizo
hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana,
kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi”
nalifafanua Dkt Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama
iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale
wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja
na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika
uchumi wa nchi.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii
chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa
usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma
alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya
maboresho ndani ya Mahakama.
Alisema
kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala
bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa
wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau
katika shughuli za mahakama.
Aidha
Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri
ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249
ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya
kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani
zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
Naye
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba
imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati
ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni
moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa
majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria
Mkuu.
#MAGAZETINI LEO# Mbowe na Naibu Spika Dr Tulia Ndani ya BIFU Jipya
Mvutano umeibuka bungeni kati ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya Mbunge huyo wa Hai kumwuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa swali lililopingwa na Naibu Spika kwa maelezo kuwa ni la kisheria si la kisera.
Sakata
hilo liliibuka asubuhi katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu,
baada ya Mbowe kuhoji sababu za Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
kusota rumande kwa kukosa dhamana, Peter Lijualikali wa Kilombero
anayetumikia kifungo cha miezi sita gerezani na wanachama wengine wa
Chadema wanaokabiliwa na mashitaka mbalimbali.
Mbowe
alimtaka kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni, aeleze kama ni
sera ya Serikali kuua vyama vya upinzani, huku akisema Rais John
Magufuli alipata kutamka kuwa atavimaliza vyama vya upinzani kabla ya
mwaka 2020.
Kwa maswali hayo, Dk Tulia alimtaka Waziri Mkuu kujibu swali linalohusu sera na kuachana na yanayogusa masuala ya kisheria.
Jambo
hilo liliwafanya wabunge wa Upinzani huku wakipiga meza kwa takribani
dakika tano kupinga, wakimtaka Naibu Spika aache Waziri Mkuu ajibu swali
hilo.
Katika
swali lake la msingi, Mbowe alisema wakati jana ikiwa ni Siku ya Haki
Duniani, imepita miezi mitatu tangu Lema aanze kusota rumande huku
akinyimwa dhamana licha ya kuwa iko wazi.
Pia
alisema Lijualikali anatumikia kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la
kisiasa sambamba na mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa wa Lindi, Suleiman
Mathew aliyefungwa miezi minane na madiwani zaidi ya sita na viongozi
wengine 215 nao wakifungwa au kuendelea na mashitaka huku zikifanyika
hila za kuidhoofisha CUF.
“Haya
yanayoendelea katika Serikali ambayo ni kinyume na utamaduni na mazoea
yetu kama Taifa, je ni utekelezaji wa sera ya kuua upinzani chini ya
Rais Magufuli?” Alihoji Mbowe.
Kabla ya Waziri Mkuu kujibu swali hilo, Dk Tulia aliingilia kati na hali kuwa hivi:
Dk Tulia:
Katika swali lako kuna masuala ya kisera na kisheria. Maswali
yanayomhusu Lema na Lijualikali na madiwani sita ni ya kisheria, hayo
kuhusu leo (jana) kuwa siku ya haki duniani, Waziri Mkuu anaweza
kuyajibu.
Majaliwa: Nakanusha,
Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani, nchi inaongozwa
kwa sheria, kanuni na taratibu na kuna Bunge, Serikali na Mahakama.
Hakuna mhimili unaoingilia mhimili mwingine. Jambo lililopo mahakamani
halizungumzwi kokote, siwezi kuzungumzia hilo.
Mbowe:
Kwa kuwa Rais anaonekana kuvunja Katiba ikiwa ni pamoja na kupiga
marufuku mikutano ya vyama vya siasa, je tukileta ushahidi kuwa Rais
amekusudia kuumaliza upinzani kabla ya 2020, Waziri Mkuu utakuwa tayari
kuwajibika kwa kujiuzulu?
Dk Tulia:
Mbowe swali lako la maelezo ya jumla, yako sawasawa ila la kumtaka
Waziri Mkuu kuwajibika si la kisera, kuwajibika si sera uliza swali la
kisera.
Mbowe: Labda
swali langu nilielekeze kwa Naibu Spika (Dk Tulia). Swali langu
lilikuwa la mwendelezo ambalo hutokana na majibu ya msingi yaliyotokea.
Kama kulikuwa na msingi wa kisera kwenye swali la msingi, swali la
mwendelezo linakwenda kutokana na majibu yaliyotolewa. Waziri Mkuu aseme
tu kama yupo tayari kujiuzulu tukileta ushahidi.
Katika
maelezo yake, Dk Tulia alitaka Mbowe ajikite katika swali la kisera
jambo ambalo Mwenyekiti huyo wa Chadema alipinga na kusisitiza kuwa
huenda mambo yanayofanyiwa wapinzani, wabunge, mawaziri Serikali
inayafurahia.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)