ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 3 Februari 2017

#MAGAZETINI LEO# Rais Magufuli aitaka Mahakama kufuatilia madeni ya kesi serikali ilizoshinda

Na Beatrice Lyimo - MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo jana  jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Alisema  kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo  Serikali imeshinda kesi hizo japo  fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
 
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
 
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.
 
Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.
 
Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
 
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.

Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kes

Hakuna maoni: