ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 8 Februari 2017

MAKONDA AITWA BUNGENI KOWAOMBA MSAMAHA WABUNGE

chanzo chetu cha habari kutoka Bungeni mjini Dodoma kinaeleza kuwa mchana wa leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alisimama na kutoa hoja binafsi akitaka Bunge kumuwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, baada ya kauli aliyotoa RC Makonda mapema leo baada ya kumaliza kutaja orodha ya watuhumiwa wengine 65 kwenye sakata la madawa ya kulevya ambapo aliulizwa swali juu ya yale yanayozungumzwa Bungeni juu ya jinsi anavyoendesha kampeni hiyo ambapo Paul Makonda alijibu kuwa hajishughulishi na kauli za wabunge kwani kazi yao ni kulala na wengine kazi zao ni kuchekesha wenzao.
Baada ya kauli hii ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mbunge wa Mkuranga amewasilisha hoja binafsi yenye mapendekezo matatu:
1. Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam aende Bungeni mjini Dodoma na awaombe msamaha Wabunge kwa kulidhalilisha Bunge hilo.
2. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akiwa kama msimamizi wa shughuli zote za serikali Bungeni atoe tamko kuhusu kauli hii iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kuliomba msamaha Bunge kwa niaba yake.
3. Bunge liandike barua kwenda Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimtaka Mkuu huyo wa mkoa aitwe kwenda Bungeni mjini Dodoma ili akaliombe msamaha Bunge kwa kauli aliyoitoa.
Abdallah Ulega, Mbunge wa Mkuranga
Baada ya kuwasilisha hoja hii, wabunge kwa pamoja walikataa hoja namba mbili ya Waziri Mkuu kuzungumza kwa niaba ya serikali au kuomba msamaha kwa kauli alizotoa Paul Makonda na badala yake wamekubaliana kuwa Bunge liandike barua kwenda kwenye Kamati ya Maadili ya Uongozi wa Umma wakitaka Mkuu huyo wa Mkoa kwenda Bungeni akaombe msamaha yeye mwenyewe.
Taarifa zinasema kwamba kufikia jioni hii barua hiyo imeshaandikwa na kutumwa kwenda Kamati ya Maadili ya Watumishi wa Umma ili kutekeleza mchakato uliopendekezwa

Hakuna maoni: