Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.
Kauli
hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali
mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa
wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni
"Nina
ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu
anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo
katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa
pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini
sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo
maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu
anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya
Uwoya
pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani
jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya
mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .
Amesema
katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanaongea uongo na hata
mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo
havimpendezi Mungu.
"Mimi
nina hofu ya Mungu sana pia napenda kusali linapokuja suala la kazi
yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu kwa sababu katika
uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu lakini ndiyo
kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha
mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.
Kwa
waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za kulevya, amewajibu kuwa
hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini
yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za
jinsia moja lakini pombe anakunywa
"Situmii
dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina
uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu
wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"
Pia
amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi, ambapo amesema
anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo ndefu, hivyo
hawezi kuvaa nguo ndefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni