ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 14 Februari 2017

HONGERA WALIMU WA NYALUMBU SEKONDARI

 
Na Mwandishi wetu, 
Katika makala yetu ya leo tunapenda kuwapongeza  walimu, wanafunzi na wafanyakazi wote wa shule ya sekondari Nyalumbu inayopatikana wilaya ya kilolo katika mji mdogo wa ilula katika kata ya Nyalumbu Kwa mafanikio yao mema katika kutoa elimu.
Kwa fursa hii, mwandishi wetu ameamua kuwapongeza na kuwatakia kazi njema yenye kuwa mfano, yenye kuleta tija na ustawi katika taaluma na maendeleo kwa ujumla.

Tunaamini, ingawaje mnakumbana na changamoto mbalimbali , bado mchango na jitihada zenu  katika taaluma zimeonekana ndani na nje ya wilaya ya kilolo.

Sanjari na kuwapongeza walimu wote katika shule hiyo, pia mwandishi wetu anawaasa walimu wengine kutoka shule nyingine kama shule ya sekondary kiheka iliyoweza kuwa miongoni mwa shule mbili za mwisho kimkoa kuiga mfano huu na kujifunza namna walimu wa shule hii walivoweza kufanikiwa kupata ufaulu mzuri katika mitihani yao.

Tunaamini ufanisi huu unaooneshwa na shule hiyo unastahiri pongezi na motisha, na hasa wilaya kutazama namna yakuwapongeza walimu hawa ili kuleta hamasa ya ushindani zaidi.
Tunawapongeza sana utawala wa shule akiwemo Mkuu wa shule(Myinga), makamu mkuu wa shule, walimu wa taaluma(mwl mwangonela J, na mwl Shonde) kwa kuweza kuongoza walimu wenu kufanya kazi nzuri ya kufundisha bila hata kuzembea tunaamini ukiwa mtawala ni Adui wa wasiofuata sheria endeleeni kufanya kazi kwa weledi huo. 
Pia kabisa tunawapongeza walimu wote kutoka Shule ya sekondari Nyalumbu kwa kuonesha ushupavu wa hali ya juu katika ufundishaji na hata kutumia muda wenu wa ziada kutoa elimu kwa wanafunzi. 
Na mwisho wanafunzi wetu kwa jitihada zenu katika masomo yenu nikiwaona wanafunzi wa shule ya sekondari Nyalumbu wamejengwa katika mazingira ya kusoma na siyo kucheza, wafundisheni wanafunzi wenzenu namna ya kusoma ili waweze kufaulu vizuri 
"mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni bila kuficha ukweli"

Hakuna maoni: