ELIZABETH
Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini jana
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya
kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App.
Akisomewa
mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya Hakimu
Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho kilicho
kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Wakili
Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa huyo
aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;
“….Rais
kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… f****l** lile,
kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi
ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”
Hata
hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa
serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Mtuhumiwa
alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila
mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni