ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 30 Aprili 2015

KUTOKA MAGAZETINI LEO TAR 30/04/2015

Mwanafunzi auawa baada ya kukutwa na barua ya mapenzi


Serikali yatangaza mikakati ya kuimarisha shilingi

WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya Salum amesema kupatikana kwa mikopo ya kibiashara yenye thamani ya dola za Marekani milioni 500 zitasaidia kupunguza kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.
Akizungumzia mwenendo wa mfumko wa bei wakati wa kuwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/16 kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana jijini Dar es Salaam, alisema serikali imekuwa ikiweka mikakati kadhaa ya kuhakikisha sarafu inaimarika.
“Napenda kuwahakikishia wabunge na wananchi kuwa Serikali inachukua hatua muhimu za kuhakikisha thamani ya Shilingi inaendelea kuimarika,” alisema.
Alisema maeneo ambayo wamepanga kutumia ni kuimarisha maeneo maalumu ya kuzalisha bidhaa za kuuza nje na maeneo maalumu ya uwekezaji kiuchumi.
“Watanzania wazitumie fursa hizi ili kuongeza mauzo nje sambamba na kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma zisizo za lazima kutoka nje,” alisema.
Mkuya alisema kumekuwapo na sababu kadhaa za kutetereka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ambazo ni kuwapo na mapato kidogo yanayotokana na mauzo ya nje kwa wastani wa mapato yanayoweza kugharamia asilimia kati ya 60 na 70 ya mahitaji kutoka nje ya nchi.
Alisema pia kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia hali ambayo imeathiri mapato yatokanayo na dhahabu kwa kiasi kikubwa.
”Kwa mfano mwaka unaoishia Januari 2015, mapato kutokana na dhahabu yalishuka kwa takribani dola za Marekani milioni 334 na hivyo kupunguza ahueni ambayo ingeweza kupatikana kwa ongezeko la mauzo ya bidhaa za viwanda pamoja na utalii."
Alisema pia ongezeko la mahitaji ya dola kwa ajili ya malipo ya gawio nje ya nchi kwa baadhi ya makampuni binafsi, ucheleweshaji wa fedha za mikopo ya kibiashara (kiasi cha dola milioni 536) katika kipindi cha miezi tisa ya kwanza ya mwaka wa fedha 2014/15.
“Matarajio yetu ni kwamba fedha kutoka nje zitaingia siku za karibuni kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina alisema sababu ya kuporomoka kwa sarafu kunatokana na Benki Kuu na serikali kwa ujumla kutokuwa na udhibiti wa matumizi ya fedha za kigeni. “Nchi nyingi zinadhibiti sana matumizi ya dola, lakini hapa kwetu unaweza kwenda kwenye duka la kubadilishia hela, hupewi risiti na hakuna udhibiti wote,” alisema.
Mpina alisema kuna haja sasa kampuni nne ambazo zina matumizi makubwa ya dola ya Tanesco, MSD, Tanroads na waagizaji wa mafuta kununua dola BoT badala ya kununua kwenye benki ya biashara.

Msajili avionya vyama vya siasa

Last Updated on 30 April 2015
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama vya siasa na wanasiasa wasikamiane na kukomoana kwa sababu, kufanya hivyo hakujengi demokrasia wala kuisaidia nchi.
Badala yake, amevielekeza viimarishe uelewano na kusaidiana, ili kujenga Tanzania yenye amani na utulivu, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya jinsi ya kufikia na kuutekeleza uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa amani, Jaji Mutungi alisema ameona dalili za wanasiasa na vyama vyao kukamiana.
Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), litakalotoa ripoti ya utendaji wa ofisi hiyo katika mkutano utakaoendelea leo jijini humo, lengo likiwa kuishauri namna ya kuboresha utendaji.
Katika mkutano huo unaohusisha wadau mbalimbali wa siasa nchini, wakiwemo wawakilishi wa vyama 22 vya siasa na taasisi tofauti, Jaji Mutungi alisema, “Tanzania ina tunu ya amani, hivyo wanasiasa wasijaribu kuivuruga kwa kuendesha siasa zisizo zingatia dhana ya demokrasia ya kweli.
Alionya kuwa uzembe wowote utakaofanywa na wanasiasa au vyama vyao unaweza kuiathiri nchi, na kuwafanya Watanzania wajute kuingia katika mfumo wa siasa za vyama vingi.
Jaji huyo alisema pia kuwa amejiridhisha kuwa baadhi ya vyama vya siasa vimeshindwa kuielewa vizuri dhana ya demokrasia ya vyama vingi, hivyo kuwa na fikra za kukamiana na kukomoana, ambazo kwa namna yoyote, hazimsaidii Mtanzania.
“Ninawaomba wanasiasa na vyama vyenu muelewe kuwa, harakati zote za kufikia uchaguzi mkuu zinapaswa kuwa na lengo la kumtafuta kiongozi atakayeiendesha nchi ifikie maendeleo. “...Sote tunajenga nyumba moja ambayo ni nchi yetu, hivyo, hatupaswi kugombania fito kwa mtindo utakaosababisha nyumba isijengwe,”Jaji Mutungi alisisitiza na kuongeza kuwa mikutano kama hiyo itaendelea kuwepo ili kupanua uelewa wa wanasiasa juu ya dhana hiyo ya demokrasia ya vyama vingi. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Philipe Poinsot aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kukuza demokrasia ya vyama vingi na kuwakumbusha wanasiasa na vyama vyao kuwa wao ndio wenye dhamana ya kuilinda demokrasia hiyo pamoja na amani iliyopo.
Alisema,”katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Tanzania imekuwa na vuguvugu linaloweza kusababisha hali ya sintofahamu kwa wananchi, jambo ambalo si jema hasa endapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu na matukio muhimu ya upigaji kura ya maoni.
Katika hatua nyingine, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idara ya Sayansi ya Siasa, Dk Benson Bana alisema, ingawa demokrasia ya vyama vingi inaonesha kuanza kufanikiwa nchini, vyama vya siasa bado vinaitekeleza vikiwa na dhana ya utengano.
back to top  


MICHEZO NA BURUDANI
  

Pluijm: Natamani kikubwa zaidi ya ubingwa VPL


NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van Der Pluijm, amesema ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kitu kidogo sana kwake, kwani bado nafsi yake inatamani kitu kikubwa zaidi kwa klabu hiyo.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1dhidi ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi uliofanyika Jumatatu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kufikisha jumla ya pointi 53, zilizopelekea klabu hiyo kutangazwa kuwa mabingwa wapya msimu huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema tayari amejipatia sifa hapa nyumbani kwa kuipa ubingwa Yanga, akieleza sasa ni wakati wa kuonyesha maajabu kimataifa.
Pluijm alisema kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, tayari mikakati yake yote ambayo alijiwekea kabla ya mchezo huo wa marudiano imekamilika.
“Ubingwa wa ligi ni kitu kidogo kwangu, hapa kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuelekeza nguvu zote kimataifa,” alisema Pluijm.
Mholanzi huyo alisema wakati anakabidhiwa kikosi cha Yanga, alijiwekea dhamira ya kuwapa ubingwa na hilo limeweza kutimia.
“Nilipokuwa naingia mkataba nilisema lazima timu ninayoifundisha ichukue kombe la ligi, bado nataka kuishuhudia ikifanya kitu kikubwa zaidi,” alisema Pluijm.
Timu hiyo inatarajiwa kuvaana na Etoile du Sahel katika mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Tayari timu hiyo imetua Tunisia kwa ajili ya mchezo huo.(SOURCE: MTANZANIA)

ZILIZOBAMBA KWENYE MAGAZETI TAR 30/04/2015

Waziri Mkuya ajikanganya


Waziri wa Fedha Saada Mkuya akiwasilisha mapendekezo ya mfumo wa Mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/16 
Na Mwandishi Wetu

Posted  Alhamisi,Aprili30  2015  saa 11:1 AM
Kwa ufupi
Juzi Mkuya alisema kuwa kipa umbele kwenye bajeti ya mwaka 2015/16 kitakuwa kwenye suala la wafanyakazi na huduma za jamii, akisisitiza kuwa bajeti haitajikita kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuwa suala hilo lilishashughulikiwa kwenye bajeti inayomalizika.


Dar es Salaam. Ndani ya saa 24, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ametoa kauli mbili zinazokinzana kuhusu fedha za Uchaguzi Mkuu baada ya juzi kuliambia gazeti hili kuwa fedha kwa ajili ya shughuli hiyo zilikwishatengwa mwaka jana, lakini jana akaziweka kwenye mapendekezo ya bajeti mpya.
Juzi Mkuya alisema kuwa kipa umbele kwenye bajeti ya mwaka 2015/16 kitakuwa kwenye suala la wafanyakazi na huduma za jamii, akisisitiza kuwa bajeti haitajikita kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuwa suala hilo lilishashughulikiwa kwenye bajeti inayomalizika.
Hata hivyo, kwenye bajeti ya 2014/15 suala la Uchaguzi Mkuu limetajwa tu na hakuonekani kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili hiyo.
Akiwasilisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Mwaka 2015/16 jana, Mkuya alisema Sh22.4 trilioni zimetengwa kwa ajili ya bajeti hiyo na kwamba Uchaguzi Mkuu umepewa kipaumbele cha kwanza kati ya vinne vilivyopo.
Hata hivyo, Waziri Mkuya hakutaja asilimia wala kiwango cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, ambao kikatiba unatakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Katika hali inayoongeza sintofahamu, Mkuya alisema moja ya mafanikio yaliyopatikana katika Bajeti ya Mwaka 2014/15 ni kufanyika kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.
Alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kukamilisha miradi inayoendelea, kuweka msukumo maalumu kwenye miradi ya umeme na maji vijijini na kuimarisha rasilimali watu.
Alisema Serikali imepanga kutumia Sh16.7 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Sh6.6 trilioni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na taasisi na Sh2.6 trilioni zitatumika kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva.
Hata hivyo, Mkuya alishindwa kuweka wazi jumla ya fedha zitakazotumika kwenye Uchaguzi Mkuu au kiasi kilichokwishatengwa kwa ajili ya kazi hiyo mpaka sasa.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuya alisema: “Bajeti hii imezingatia pia maandalizi ya Katiba Mpya, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.”
Mapendekezo ya matumizi ya kawaida ya Serikali kwa mwaka 205/16 pia yanaonyesha kuwa Mfuko Mkuu wa Serikali utatumia Sh6.3trilioni, matumizi mengineyo wizarani Sh3.4 trilioni, matumizi mengineyo mikoani Sh83 bilioni na matumizi mengineyo Mamlaka za Serikali za Mitaa Sh208 bilioni.(source mwananchi)


Sumatra wasitisha nauli mpya kwa siku 14

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesitisha kwa siku 14 utozaji wa nauli mpya za mikoani zilizokuwa zianze leo baada ya kupata maombi ya rejea kutoka kwa wamiliki wa mabasi ya mikoani kutaka kuangaliwa upya nauli hizo zilizoshushwa.
Kutokana na hatua hiyo, wamiliki wa mabasi ambao jana walipanga kugoma walisitisha uamuzi huo hadi hapo serikali itakapotoa uamuzi kutokana na malalamiko yake hayo.
Aprili 15 mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli ambavyo vilitarajiwa kuanza leo Aprili 30, mwaka huu kwa kushusha nauli za mabasi ya mikoani huku nauli za mijini za daladala zikibaki palepale.
Kwa mujibu wa kanuni za tozo za mwaka 2009 uamuzi kuhusu nauli hizo utafanyika baada ya siku 14 baada ya kusikiliza malalamiko yao na kamati maalum na kisha kutolewa maamuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Giliard Ngewe aliliambia gazeti hili kuwa walipokea barua ya maombi ya rejea jana (juzi) ambayo ilikuwa siku 14 kisheria kwa wamiliki kupinga nauli hizo ka maandishi, na kama siku hiyo ingepita wasingesikilizwa.
Naye Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu alisema Serikali imetoa wiki mbili kwa Wamiliki wa Mabasi yaendayo mkoani (Taboa), kupeleka hoja yahesabu kwa nini wanasema nauli isishushwe.
Alisema tangu nauli ziliposhushwa mafuta na dola yameendelea kupanda.
“Tukishusha sisi ndio tutakaoumia kwa sababu hatuna duka letu la tairi, vipuri wala mafuta yetu wenyewe ambayo hayatatozwa kodi,” alisema.
Imeandikwa na Anastazia Anyimike na Lucy Ngowi (Chanzo:Habari leo)

Rukwa wakamata bunduki 50, risasi 768

JESHI la Polisi mkoani Rukwa limewakamata watuhumiwa 50 na silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki 48 , risasi 768 na maganda ya risasi 101.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Namanyere alionesha silaha hizo na risasi zake haradharani mbele ya waandishi wa habari.
Kamanda Mwaruanda aliongeza kuwa watuhumiwa hao na silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo ya Namanyere na kijiji cha Kirando mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani humo iliyofanyika kati ya Aprili 18 na 27 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa Polisi mkoani humo, kikosi kazi taifa na askari wa wanyamapori wa pori la akiba la Lwafi wilayani Nkasi.
Alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni bunduki aina ya AK 47 yenye namba 1162416 na risasi zake 409, bunduki nane aina ya rifle na risasi zake 83, bunduki 19 aina ya shotgun na risasi zake 138, bastola tano na risasi zake 133 na magobori 15.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na maganda ya risasi aina ya shotgun 96, maganda ya risasi aina ya rifle tano, magazini za bunduki aina ya SMG nne na vifaa vya kutengeneza bunduki za kienyeji ‘magobori’ mitutu sita.( chanzo:Habari leo)

Wanazuoni wajadili mustakbali wa Tanzania ndani ya demokrasia ya vyama vyingi

Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria vipo.

Dk Bana alisema kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.

Alisema watu kama wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.

Katika shauri hilo la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning) ili iweze kukabiliana navyo mapema.

Akizungumzia kama Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23 iliyopita.

Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahalo
Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.
Aidha alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.

Alisema mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.

Pia alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk bana akizungumza katika mdahalo
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.

Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.

Alisema kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa vyama vingi.

Alisema pia kuna haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu yanayostahili katika maeneo yao.
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .

Alizungumzia pia haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.

Katika mdahalo huo ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa changamoto za siasa za vyama vingi.

Profesa Rugumamu alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
IMG_4917
Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Miongoni mwa changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi, wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.

Pia alizungumza uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.

Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.

Awali akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na kutokuelewana.

Alisema mkutano huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.

Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.

Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.

Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.

Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumza
Profesa Rugumamu akizungumza.
IMG_4861
Baadhi ya washiriki( SOURCE ZANZIBAR NEWS)


Jumatatu, 27 Aprili 2015

Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015 Zimetoka......Bofya Hapa Kuona Majina



 

 
A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
 
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
 
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
 
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
 
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari


B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
 
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
 
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
 
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
 
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
 
v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
 
Bonyeza  Hapo Chini Kuona  Orodha  Ya  Majina:

 
 

Jumamosi, 25 Aprili 2015

ACT-Tanzania yabadili jina.

ACT-Tanzania yabadili jina.

t
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto.
Chama kipya cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (pichani juu), kimebadili jina lake la awali la ACT-Tanzania.
 
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imekubali maombi ya chama hicho huku ikiwataka kurudisha cheti cha usajili wa awali na kupewa cheti kingine.
 
Awali ACTL-Wazalendo ilipata usajili kwa jina la ACT-Tanzania na baadae kuomba kulibadili jina hilo.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ameridhika na maelezo yaliyokuwa yametolewa na uongozi wa chama hicho wa sababu za kuamua kubadili jina la chama hicho kutoka ACT-Tanzania hadi ACT-Wazalendo.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari jana jiijini Dar es Salaam, Jaji Mutungu alijibu ombi hilo kwa njia ya barua.
 
Katika taarifa hiyo inaeleza: "Nikurejeshe kwenye barua yenye kumbukumbua namba AC-HQ/MSJ/2015 ya Aprili 15, mwaka 2015 ikisomwa sambamba na barua yangu yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/80 ya Aprili 13, mwaka 2015 kuhusu suala tajwa hapo juu".
 
Jaji Mutungi alieleza kuwa, alisoma na kuyatafakari kwa kina maelezo katika barua ya ACT-Wazalendo, na kwamba ameridhika na maelezo yao kuhusu jina jipya la chama hicho kwa mujibu wa  kanuni ya 7 ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa.

Ijumaa, 24 Aprili 2015

SIMULIZI FUPI YA MAPENZI


 

Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa. 


Akiwa nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake. 



Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo, aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa (mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema "Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana." Yule dada alitabasamu na kusema "Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito wangu, samahani kwa usumbufu wangu".
Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza "Hakuna tatizo, usijali kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina...." Kabla hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula kungu "Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri, nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda" Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema "Chochote tu, zawadi ni zawadi, alimradi kuwe na mapenzi ya kweli" Dada yule alitabasamu na kusema "Ni kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi, nitampenda maisha yangu yote" Kaka yule akauliza "Utampenda? Nani huyo"
.
 Yule dada alitabasamu tena na kusema "Samahani, rafiki nilikuwa sijakuambia, wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi, nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia" Yule kaka alibaki amepigwa na butwaa, "Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo." Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita ili ampatie kadi bila ya mafanikio.
by ADELA

Factory Discipline in the Industrial Revolution.1

Jumatano, 22 Aprili 2015

SIASA NI MCHEZO





  






Kwani kuna ambaye hajui kama bajeti ya nchi yetu inapitishwa na wanasiasa? Kuna asiyetambua kwamba kilimo kinachoitwa uti wa mgongo wa taifa hili nacho kinasimamiwa zaidi na wanasiasa? Hivi kweli kabisa huenda akatokea mtu aseme kuwa hajui kama elimu yetu ipo chini ya uangalizi na usimamizi wa wanasiasa?

Jamani!Hata ulinzi na usalama wetu nao hatujui kama upo chini ya himaya ya mwanasiasa? Hapana, huyu ni lazima nimtaje. Yeye ndiye amiri jeshi mkuu anayepigiwa saluti na wanausalama wote. Ndio mpaka afya zetu wanaopitisha bajeti yake ni wanasiasa tu na sio wengine. Hakuna kinachofanyika chini ya jua la nchi yetu lisiwe na mkono wa wanasiasa kwa sababu bajeti nzima inapitishwa na haohao.

Kifupi tunaweza kusema kwamba maisha yetu yote yapo chini ya mwamvuli wa siasa na kwa maana hiyo tusiifanyie mzaha. Ndio, tusicheze kabisa na siasa kwa sababu tutakuwa tunachezea maisha yetu wenyewe. Kwani si mnajua kama katiba ya nchi ambayo ndio sheria mama nayo miongoni mwa walioitunga na kuipitisha ni wanasiasa?

Hata katiba inayopendekezwa, wanasiasa walikwuwepo nahata jengo lililotumika ni lilelile linalotumiwa na wanasiasa kila uchao na uchwao. Si utani jamani siasa ndio yenye nguvu na nafasi kubwa kuliko chochote Tanzania na ndio maana hata wanataaluma bobezi nao hawashikiki kwenye siasa. Huko kuna ‘mshiko’ wa maana hata kama pakiwa kuna fujo na vurugu.

Lakini hata hivyo ukiachana na nafasi iliyokuwa nayo siasa hapa nchini, bado hatuwezi kuacha kusema kuwa ni mchezo mchafu. Mara ngapi mfano kule bungeni kumetokea vurugu? Nani hakuwahi kushuhudia washa zima maikrofoni inayofanywa na waheshimiwa wanasiasa (wabunge) ambao ndio tumewaamini wakatuwakilishe? Ni kweli tumewatuma wakaropoke au kupiga kelele zisizokuwa na natija kwetu? 
Tumewatuma wakatetee maslahi ya vyama vyao na matumbo yao?

Tukubali tu kwamba siasa ni mchezo mchafu unaowachafua wengi, wake kwa waume na vijana kwa wazee. Imechafua upande wa vyama vya upinzani na chama tawala. Inawachafua wasomi wetu na wanataaluma waliofurika huko.

Mtangazaji wa masuala ya siasa John Calvin Thomas (Cal Thomas) aliyezaliwa Disemba 2, 1942 katika jimbo la Washington D.C nchini Marekani,anasema kuwa sababu mojawapo ya watu kuichukia siasa ni kwamba ukweli ni mara chache kuwa lengo la mwanasiasa. Hii ina maana kuwa wanasiasa wengi kama sio wote hawaupi ukweli nafasi yake hasa kwenye malengo yao ya kisiasa mbele ya wananchi.