SHAMRA SHAMRA ZA USHINDI
Baada ya kampeni zilizo
dumu kwa wiki moja, wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam kitivo cha
uwalimu Iringa (MUCE) wamefanya uchaguzi leo, Kwa hali ya amani na utulivu wa hali ya juu na hatimaye kuwapata
viongozi wa serikali yao, Uchaguzi huo uliokuwa unawagombea zaidi wawili katika kila nafasi ulilazimu kuwachukuwa siku nzima kufanyika na
hatimaye Bw. BAKARI, IBRAHIMU ameibuka mshindi katika nafasi ya urais, Kwa matokeo mengine ungana nasi kesho
Alhamisi, 7 Mei 2015
Mrema avuliwa uanachama TLP
Mrema avuliwa uanachama TLP
NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema.
Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na MTANZANIA Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa yakimuhusu Mrema, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine waliovuliwa uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria, Dominata Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley Temba.
Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009 ibara 9.5(c).
Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, alipotafutwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema kamati hiyo haitambuliki kisheria.
“Kamati hiyo haitambuliki kisheria, na hata Mrema mwenyewe amekuwa akipinga TLP kuwa na kamati ya aina hiyo na hata viongozi wake hawatambuliki, ” alisema(Chanzo Mtanzania)
Jumanne, 5 Mei 2015
Madereva wasitisha mgomo, mabasi ya mikoani yaanza kazi
Na Online Team, Mwananchi
Posted Jumanne,Mei5 2015 saa 8:24 AM
Posted Jumanne,Mei5 2015 saa 8:24 AM
Kwa ufupi
Mgomo huo ulioanza jana umesababisha usumbufu mkubwa
kwa raia sehemu nyingi nchini Tanzania ambao walikuwa wamejiandaa
kusafiri kuelekea katika mikoa mingine jana na leo kwa ajili ya shughuli
zao mbalimbali zikiwemo za kibiashara na kijamii.
Hatimaye madereva wa mabasi na malori wameamua
kusitisha mgomo leo baada ya Serikali kuwahakikishia kuwa inaandaa
utaratibu mzuri wa kujibu na kushughulikia matatizo yao.
Mgomo huo ulioanza jana umesababisha usumbufu
mkubwa kwa raia sehemu nyingi nchini Tanzania ambao walikuwa wamejiandaa
kusafiri kuelekea katika mikoa mingine jana na leo kwa ajili ya
shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kibiashara na kijamii.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Paul Makonda akiwa na viongozi wengine wa Serikali walifika
katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha ubungo na kuzungumza na
madereva hao wakiwataka wasitishe mgomo wao na kuanza kazi kwani mambo
yao Serikali inayafanyia kazi na hivi karibuni watajibiwa.
Kufuatia hali hiyo maderva hao walikubaliana na
ombi hilo la Serikali baada ya kutokea kwa Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe ambaye naye aliwasihi waache mgomo
huo kwani Serikali itafanyia kazi maombi yao.
Nchi yasimama: Madereva mabasi, malori wagoma sehemu kubwa ya Tanzania
Dar/mikoani. Nchi imesimama. Hii ndiyo sentensi
inayofaa kuelezea tukio la jana la mgomo wa madereva nchini kote ambao
kwa mara ya kwanza ulisababisha mabasi yote kutoka Dar es Salaam kwenda
mikoani na nchi jirani kushindwa kuondoka.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), kushindwa kutoa huduma kwa sababu yoyote ile.
Tangu asubuhi hadi jioni, hakuna basi hata moja
lililotoka wala kuingia katika kituo hicho hadi abiria walipoanza kukata
tamaa na baadhi yao kuondoka na wengine kuanza kushinikiza kurejeshewa
nauli.
Mgomo huo ambao ni mwendelezo wa ule uliofanyika
Aprili 9, mwaka huu ulipewa uzito na madereva hao baada ya ahadi
walizopewa na Serikali kutofanyiwa kazi kama ilivyoahidiwa na Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.
Hata hivyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameunda kamati ya
iliyotangazwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ya kusimamia usafiri
barabarani itakayowakutanisha wadau wote ili kutatua matatizo katika
sekta hiyo kila yanapotokea.
Polisi wachemsha Dar
Tangu saa 2.30 asubuhi, polisi walijaribu
kuyasindikiza mabasi waliyodhani madereva wake wako tayari kuondoka
Ubungo lakini walishindwa baada ya kutoungwa mkono.
Mkuu wa Trafiki Ubungo, Inspekta Yussuf Kamotta
akiwa na Inspekta Solomon Nkindwa ambaye pia ni mkaguzi wa magari,
waliingia katika basi la Kampuni ya Master City na kuliondoa kituoni
hapo wakiwa na mmiliki wa kampuni hiyo, Abdallah Mohammed huku
wakimtafuta dereva bila mafanikio na kulazimika kulitafutia sehemu
salama ya kuliegesha baada ya madereva kulizingira.
Kitendo cha askari hao kilisababisha kuzomewa kwa
Inspekta Nkindwa wakisema mkaguzi huyo arudi shule akasome...
“Solomoooon… rudi shuuuule… gia nane… zimekushinda,” walisikika madereva
hao wakiimba huku wakikimbia mchakamchaka kurudi zilipo ofisi zao.
Kutokana na vurugu zilizotokea nje ya kituo hicho,
polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu
waliokuwa katika makundi.
Nje ya UBT, magari sita ya polisi yaliegeshwa
katika makutano ya barabara za Sam Nujoma, Nelson Mandela na Morogoro
wakati mengine yakielekea Mwenge na Buguruni kwenda kukabiliana na
tishio lolote ambalo lingeweza kutokea.
Saa 5.30 askari wa Kikosi cha Mbwa waliwasili
kuongeza nguvu na kuvutia macho ya wengi kutokana na jinsi walivyokuwa
na pilikapilika bila ya kuwapo kwa mhalifu yeyote anayetafutwa.
Sikukuu ya madereva
Tofauti na migomo mingine, huu haukuwa na vurugu
zozote wala sintofahamu kwani kila mtu aliyekuwa UBT alionekana akiwa
katika sehemu yake akiendelea na hamsini zake. Abiria walikuwa katika
mabasi husika huku mawakala na makarani wakiendelea kukatisha tiketi za
safari na kupanga mizigo ya abiria.
Huku wakiendelea na mazungumzo yao katika vikundi
katika kituo hicho, madereva hao walisikia wakisema hapakuwa na mgomo,
bali sikukuu yao.(CHANZO MWANANCHI)
ANGALIZO ..............
Ndugu watazamaji wa blog hii, blog hii imeanzishwa kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii,kutoa taarifa na kuonya, kutoa maoni na kama unatangazo lolote huna budi kuwasiliana nasi
lakini sio kutaka kile wanachokitaka watu wachache kwa hiyo kama kuna tatizo wasiliana nasi na si kulaumu na kuchafua chombo husika, .
TANGAZA BIASHARA, TAARIFA NA MAELEZO WASILIANA NASI.
Jumamosi, 2 Mei 2015
KAMPENI ZA UCHAGUZI KUTOKA CHUO KIKUU KISHIRIKI MKWAWA 2015
KAMPENI ZA UCHAGUZI KUWANIA UONGOZI KATIKA SERIKALI YA WANAFUNZI ZAENDELEA KWA MBWEMBWE
Serikali ya wanafunzi ya Chuo
Kikuu cha Mkwawa (DARUSO-MUCE) imemaliza muda wake na hivyo iko katika mchakato
wa kutafuta Rais mpya wa serikali hiyo pamoja na wabunge watakaongoza
serikali hiyo kwa kipindi cha 2015/16 Chuoni hapo.
Aidha kampeni za mgombea Urais
ndugu BAKARI, IBRAHIMU zimeonekana kuwawavutia wanafunzi wengi kwani
amekuwa akitembelea wapiga kura wake huku akiwa ameandamana na wafuasi
wake ambao wamekuwa wakimlinda kila anapokwenda. Aidha mgombea huyo Bw. BAKARI, IBRAHIMU ndie ambae anaonekana ni mwenye asilimia kubwa ya kuweza
kushinda katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki lijalo chuoni hapo. Wagembea wengine ni; MSUYA, FAROUK na Bw MABULA
WAGOMBEA URAIS DARUSO MUCE 2015/2016.....................
Na kwa upande wa makamu wa rais wagombea wawili wamejitokeza akiwamo dada ISSASSI SUZANI na KIBONA FAUSTA katika nafasi hii ushindani unaonekana kuwa ni mkubwa sana kwani wote wana watu weng wanaowapigania ili kupata nafasi hiyo
WAGOMBEA WA NAFASI YA MAKAMU WA RAIS DARUSO-MUCE 2015/2016
Mgombea wa nafasi ya Rais Bwana BAKARI, IBRAHIMU sera
zake kwa wapiga kura (hawapo pichani) ambapo alisema katika uongozi wake
ataanza kushughulikia mikopo kwa wanafunzi wa MUCE.
Pia amesema kama atapewa nafasi hiyo
atakuwa na utaratibu wa kuwakutanisha wanafunzi wa MUCE kuanzia mwaka wa
kwanza mpaka wa tatu na wataalumu waliopo katika fani zao, lengo likiwa
ni kuwaongezea uzoefu zaidi na kujua changamoto ya kazi za kitaaluma chuoni hapo.
Aidha aliongeza kuwa atahakikisha usiri wa matokeo utaboreshwa chuoni hapo, huku akimwaga ahadi ya hakuna tatizo ambalo hawezi kulishughurikia akiwa rais na hii ilikuja baada ya mheshimiwa kitako kumuuliza mgombea matatizo gani manne(4) hawezi kuwasaidia wanachuo akiwa madarakani.
Wanafunzi hao wameonekana wana ukomavu mkubwa wa kisiasa kwani wanasikiliza kwa makini sera za wagombea na kuuliza maswali mazuri.
Cha kufurahisha ni kelele za filimbi na mayowe ambayo yametwala kila kona huku wagombea wakishangiliwa na mashabiki wao.
Nafasi
zinazowaniwa katika Uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Rais, Makamu wa
Rais, pamoja na wawakilishi wa Vitivo (wabunge) na wawakilishi wa
Maeneo (wabunge wa makazi) ambao wote watapigiwa kura.
Wagombea
mbalimbali wamekuwa wakipita hapa na pale ikiwa ni pamoja na kubandika
picha zao katika kuta ikiwa ni sehemu ya kutafuta kura.
Kwa upande wa MSUYA naye amenadi sera sake moja ya mipango yake ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wanafunzi likiwemo tatizo la maji na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara, huku akiwasii wanafunzi kuangalia hali ya chou sasa kwamba kinahitaji mtu makini anayejua matatizo ya wanachuo wote na kuwatumikia.
KWA UPANDE WA MAKAMU WA RAIS SERA ZAO IMEONEKANA KWENDA SAMBAMBA NA MARAIS lengo kubwa ni kuboresha taaluma na mazingira y chuoni hapo.
Kwa upande wake Rais
anayemaliza muda wake Bwana AGUSTINO ALFA ameishukuru tume ya uchaguzi
kwa mchakato mzima na anafurahi kumaliza muda wake
na kuwataka watakaopata nafasi za kuongoza wazingatie sheria, demokrasia
na upendo ili kuleta mshikamano katika chuo, ili wanaoongozwa wajisikie
kuwa na amani kuwepo chuoni hapo badala ya kutatua migogoro isiyokuwa
na maana. Pia ameshauri wanachuo kusikiliza sera za wagombea kwa umakini mkubwa ili kuepuka KUUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA.
MSHAURI WA WANAFUNZI ALITUMIA FURSA HIYO KUWAASA WAGOMBEA KUTUNZA MAZINGIRA HASA KUTOBANDIKA MABANGO SEHEMU ZISIZO RASMI
NAYE MAKAMU WA CHUO AKASEMA;
Makamu mkuu wa chuo amewatakia wanafunzi kampeni njema zenye baraka na fanaka na zinazozingatia sheria na taratibu za chuo.
Ijumaa, 1 Mei 2015
HARAKATI ZA UCHAGUZI DARUSO-MUCE 2015
Harakati za kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha dare es salaam, kitivo cha ualimu MUCE-Iringa wameanza kampeni za kutafuta viongozi wa DARUSO (Dar es salaam University Students Organization) mwaka 2015/2016, Uchaguzi utafanyika wiki moja ijayo chuoni hapo, Hali ya kampeni hizo ni shwari na wagombea wote tayari wameshaanza kampeni zao kwaajili ya nafasi mbalimbali
Tunaendelea kufuatilia sea za wagombea tutawaletea hiv karibuni
moja ya mgombea wa nafasi ya makamu
ANGALIA MABADILIKO YA AJIRA ZA WALIMU HAPA
Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015.
30th Of April,2015.
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa.
kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo:
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)