RAIS
Jakaya Kikwete ameagiza Wakuu wa Mikoa na Maofisa Elimu wote nchini,
kuanza ujenzi wa shule maalumu za kidato cha tano na sita kwa kila kata
na wakishindwa, katika shule za sekondari za kata, wachague baadhi na
kujenga madarasa ya vidato hivyo.
Alitoa agizo hilo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu,
yaliyoadhimishwa kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na
kuwakumbusha kuwa kati ya wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha tano
mwaka huu, ni asilimia 75 tu walioendelea na masomo hayo.
“Wakuu wa mikoa na maofisa elimu mliopo hapa naagiza na hili ni kwa nchi
nzima, tuanze utaratibu wa kuwa na shule za kidato cha tano na sita za
kata. Mnaweza kujenga shule mpya, au mchague baadhi ya sekondari za kata
ziwe na kidato cha tano na sita,” alisema Rais Kikwete na kuongeza
kusema si vyema kuwaacha mtaani asilimia 25 wenye sifa ya kuingia kidato
cha tano.
Alisema bila kuchukua hatua hiyo, Tanzania inaweza kurudi katika hali ya
elimu aliyoikuta ambapo wanafunzi wenye sifa ya kuendelea na masomo,
waliachwa kutokana na ufinyu wa nafasi za kuendelea na elimu.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakati alipokuwa akiingia madarakani,
alikuta asilimia sita tu ya wanafunzi waliokuwa wamefanya Mtihani wa
Taifa wa Darasa la Saba, ndio waliokuwa wakichaguliwa kuendelea na elimu
ya sekondari.
“Leo kila anayefaulu darasa la saba, anakwenda sekondari… tukisema leo
mwanafunzi amefeli darasa la saba amefeli kweli tofauti na zamani ambapo
walikuwa wakichaguliwa,” alisema Rais Kikwete.
Tanzania ilipotoka Rais Kikwete alielezea sababu ya Serikali inayomaliza
muda wake kuwekeza zaidi katika elimu, kiasi kwamba bajeti ya elimu
katika Mwaka wa Fedha unaoisha kuwa kubwa kuliko ya sekta zingine,
inayofikia Sh trilioni 3.4 kutoka Sh bilioni 600 iliyokuwepo mwaka 2005.
Sababu ya kwanza Rais Kikwete alisema, waliona kuwa kuwekeza katika
elimu ndio kuwekeza katika taifa na Serikali isingechukua uamuzi huo,
Watanzania hawataweza kutawala mazingira yao na kutumia vizuri
rasilimali zao.
Pili alisema alipoingia madarakani, alikuta Tanzania yenye watu wengi
zaidi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iko nyuma
ikilinganishwa na Kenya na Uganda, kwa idadi ya wanafunzi waliokuwa
wakisoma shule za sekondari na vyuo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, mwaka 2005 wanafunzi waliokuwa wakisoma
sekondari ni zaidi ya 500,000, wakati nchini Uganda waliokuwa wakisoma
sekondari walikuwa zaidi ya 700,000 na Kenya zaidi ya 900,000.
Kwa upande wa vyuo vikuu, Tanzania ilikuwa na wanafunzi 40,000 tu wakati Uganda ilikuwa na wanafunzi 124,000 na Kenya 180,000.
“Kuwa nyuma katika kutoa fursa ya elimu ikilinganishwa na wenzetu
ilikuwa inaweka nchi yetu katika mazingira mabaya katika ushindani wa
soko la ajira la Afrika Mashariki,” alisema Rais Kikwete.
Mbali na mazingira mabaya katika ushindani wa soko la Afrika Mashariki,
Rais Kikwete alisema Watanzania nao walifikia hatua ya kuamua kupeleka
watoto wao kwenda kusoma Kenya na Uganda.
Hatua zilizochukuliwa, Rais Kikwete alisema Serikali kwa kushirikiana na
wananchi, waliamua kujenga shule za sekondari za kata, ambapo wananchi
walihamasishwa, wakahamasika wakajenga shule mpaka Mkurugenzi mmoja wa
elimu, akahofia kukosa walimu wa kupeleka katika shule hizo.
“Tulihimiza wadau wengine wajenge vyuo vya elimu ya juu na kuamua mikopo
ya elimu ya juu itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vyote,” alisema Rais
Kikwete.
Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania ina wanafunzi 1,800,000 wanaosoma
sekondari na imeshaipita Uganda yenye wanafunzi 1,700,000 wanaosoma
elimu ya sekondari, lakini imezidiwa na Kenya ambayo ina wanafunzi
2,100,000.
Hata hivyo alisema ni rahisi kuipita Kenya kwa hilo pengo la wanafunzi
300,000, kwa kuwa shule za sekondari zilizopo zina nafasi ya kuongeza
wanafunzi milioni mbili zaidi.
“Hapa lazima tuwafukuzie Wakenya, lazima tuwakute na kuwapita na huu ni
ushindani mzuri kwa kuwa ni ushindani wa maendeleo,” alisema Rais
Kikwete.
Kwa upande wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema vyuo vikuu vimeongezeka
kutoka 26 mwaka 2005 hadi kufikia 52 na idadi ya wanafunzi walio katika
vyuo vikuu ilitoka 40,719 hadi kufikia 200,956.
Chanzo: Habari Leo
Jumamosi, 16 Mei 2015
Jumatano, 13 Mei 2015
NEC sasa yaanza kugawa majimbo
- BY HALIMA MLACHA
- HITS
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza rasmi mchakato wa kugawa majimbo ya uchaguzi nchini ambapo inatarajia kuanza uchunguzi wa mipaka ya majimbo hayo hivi karibuni, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Aidha, tume hiyo imesisitiza kuwa uchaguzi mkuu lazima ufanyike Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa Katiba, na kufafanua kuwa kwa mujibu wa ratiba ya uandikishaji wapigakura kwenye daftari la wapigakura, uandikishaji huo unatarajiwa kukamilika Julai mwishoni au Agosti mwanzoni mwaka huu.
Akifungua mkutano baina ya tume hiyo na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Damian Lubuva, alisema uchaguzi na mgawanyo huo wa majimbo unafanyika chini ya Katiba ya sasa ya mwaka 1977.
“Tume inapenda kuwahakikishia kuwa ugawaji huu wa majimbo utakamilika kwa wakati na wananchi watajulishwa ili vyama vya siasa viweze kuteua wagombea katika majimbo hayo,” alisisitiza Jaji Lubuva.
Alisema kwa sasa utaratibu wa kuandikisha wananchi kwenye daftari hilo la kudumu la wapigakura unaendelea vizuri na Serikali imeshatoa fedha zote za ununuzi wa vifaa vya kuandikishia zikiwemo BVR kits.
Alisema hadi sasa jumla ya BVR 4,800 zimeshawasili na zinaendelea kutumika katika uandikishiaji na Mei 20, mwaka huu BVR kits 1,600 zinatarajiwa kuwasili na Mei 29, mwaka huu pia BVR 1,520 zitawasili kwa ajili ya uandikishaji.
Alisema ratiba ya uandikishaji tayari imeshatoka na kwamba kwa sasa tume hiyo inaendelea kuandikisha ambapo Mei 19, mwaka huu tume hiyo itaandikisha wananchi wa mikoa ya Singida, Tabora, Igoma na Kagera na kufuatiwa na mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu.
Aidha pia ratiba hiyo inaonesha baada ya mikoa hiyo, uandikishaji utaendelea katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Zanzibar na kumalizikia mkoani Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alitaja vigezo vitakavyotumika kugawa jimbo kuwa ni mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu ambao utazingatia takwimu za idadi ya watu kutoka Ofisi ya Takwimu (NBS) na idadi ya majimbo ambayo kwa sasa ni 239.
“Kwa mujibu wa makadirio ya ofisi ya takwimu Watanzania wote Tanzania bara wamefikia milioni 47.1, kwa upande wa majimbo ya mjini yana watu takribani milioni 10 na vijijini watu milioni 37,” alisema Malaba.
Alisema kutokana na takwimu hizo, mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu kwa majimbo ya mjini utazingatia watu 325,000 na kwa upande wa majimbo ya vijijini wastani utakuwa ni watu 250,000, hivyo majimbo yatakayogawanywa ni yale yenye idadi ya watu zaidi ya mgawanyo huo.
Alitaja vigezo kingine kuwa ni upatikanaji wa mawasiliano kama vile barabara, simu na vyombo vya habari, hali ya kijiografia kwa mfano maeneo ya mlimani, visiwani au mabondeni ni kigezo kingine cha mgawanyo wa jimbo pamoja na hali ya uchumi.
Kigezo kingine ni ukubwa wa eneo la jimbo husika, mipaka ya kiutawala, jimbo moja lisiwe ndani ya wilaya au halmashauri mbili ambapo endapo kwa sasa zipo wilaya au halmashauri zilizogawanywa, tayari zimeshatoa mgawanyo wa majimbo.
Aidha kigezo kingine ni kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili, mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo, mazingira ya muungano, uwezo wa ukumbi wa Bunge na viti maalum vya wanawake ambavyo kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya mwaka 1977 imetenga zaidi ya asilimia 30 ya viti vya ubunge kwa ajili ya wanawake.
Alisema tume hiyo inatarajia kukutana na wadau na kujadiliana juu ya vigezo na utaratibu utakaotumika kuchunguza mipaka na kugawa majimbo, kupokea maombi na mapendekezo ya kugawa, kurekebisha mipaka au kubadili majina ya majimbo kutoka kwa wadau na kuainisha maombi hayo.
Malaba alisema tume hiyo imeweka utaratibu wa wadau kuwasilisha maombi ya kurekebisha mipaka na kugawa majimbo au kubadili majina ya majimbo ambayo yatawasilishwa kwa mkurugenzi wa halmashauri husika na kujadiliwa na vikao rasmi.
“Mkurugenzi atawasilisha maombi au mapendekezo hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye atayawasilisha katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ili kupata maoni zaidi na mwisho Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha maoni hayo kwa NEC,” alisisitiza.
Kwa upande wake Kamishna wa Tume, Profesa Amone Chaligha, alisema tume hiyo inatarajia kutoa ratiba kamili ya ugawaji wa majimbio hayo na matangazo yake kesho ili suala hilo, litekelezwe mapema iwezekanavyo.
Nao wawakilishi wa vyama vya siasa, akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na Mwenyekiti wa chama cha NLD, waliitaka tume hiyo, kuweka wazi ratiba zote zinazoendana na mchakato wa uchaguzi, ili vyama hivyo vijiandae vyema.(HABARI LEO)
welcome small city ILULA- HOME OF HOSPITALITY
Population of Ilula: | 29 193 people |
Latitude of Ilula: | -7,6833 (740'59.988"S) |
Longitude of Ilula: | 36,0333 (361'59.880"E) |
Altitude of Ilula: | 1 505 m |
Article: Tanzania | Biggest cities: Tanzania |
Photos, pictures: Tanzania | All cities: Tanzania |
The biggest cities of the World | |
GMT time in Ilula: | +3 hours |
Distance from city Ilula to 25 biggest cities of country: Tanzania
Distance (Km) | |
Ilula - Dar Es Salaam | 372 km |
Ilula - Unguja Ukuu | 398 km |
Ilula - Mwanza | 671 km |
Ilula - Zanzibar | 387 km |
Ilula - Arusha | 485 km |
Ilula - Mbeya | 315 km |
Ilula - Morogoro | 204 km |
Ilula - Tanga | 447 km |
Ilula - Dodoma | 170 km |
Ilula - Kigoma | 774 km |
Ilula - Moshi | 503 km |
Ilula - Moschi | 503 km |
Ilula - Tabora | 464 km |
Ilula - Songea | 336 km |
Ilula - Musoma | 731 km |
Ilula - Mazama | 731 km |
Ilula - Iringa | 38 km |
Ilula - Katumba | 317 km |
Ilula - Shinyanga | 531 km |
Ilula - Mtwara | 539 km |
Ilula - Ushirombo | 648 km |
Ilula - Kilossa | 141 km |
Ilula - Sumbawanga | 488 km |
Ilula - Bagamoyo | 346 km |
Ilula - Bagamojo | 346 km |
Distance from city: Ilula to Top 10 cities of the world
Distance (Km) | |
Ilula - Berlin | 6 992 km |
Ilula - London | 7 385 km |
Ilula - Los Angeles | 16 065 km |
Ilula - Moscow | 6 973 km |
Ilula - New York | 12 262 km |
Ilula - Paris | 7 034 km |
Ilula - Peking | 9 691 km |
Ilula - Rio De Janeiro | 8 565 km |
Ilula - Sydney | 11 806 km |
Ilula - Tokyo | 11 679 km |
Ilula - Prague | 6 761 km |
Jumatatu, 11 Mei 2015
Simba yaridhika Kagame na nafasi ya tatu
11 May2015
KOCHA Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema anashukuru kumaliza ligi katika nafasi ya tatu na sasa anasubiri hatima yake.
Simba ilimaliza ligi juzi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kumaliza ya tatu ikiwa na pointi 47.
Kopunovic alianza kuiongoza Simba mwishoni mwa raundi ya kwanza akichukua mikoba ya Patrick Phiri aliyetupiwa virago baada ya timu kutopata matokeo mazuri.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kopunovic alisema ligi ilikuwa na changamoto nyingi na kumaliza nafasi ya tatu ni jambo la kushukuru.
“Halikuwa lengo letu, wote tulitaka kutwaa nafasi kubwa zaidi, lakini ligi ilikuwa na changamoto nyingi, nitakabidhi ripoti yangu kwa uongozi, hapo ndipo utajua hatima yangu,” alisema kocha huyo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba.
Akilizungumzia hilo, msemaji wa Simba Haji Manara alisema wanachokisubiri ni kuona ripoti ya kocha huyo kabla ya kufanya uamuzi mwingine.
“Watu wana papara ya kutaka kujua nini kitafuata, tumeshiriki ligi kama timu nyingine na yaliyotokea yametokea, kiutaratibu tunasubiri ripoti ya kocha ndipo mambo mengine yafuate kama kusajili ama la,” alisema.
“Tunataka tuwe na uhakika wa nini tunataka kufanya, kama mabadiliko ni yapi, yote hayo tunayafanya kwa muongozo wa ripoti ya kocha,” alisema Manara.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema, Simba imepania kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kumaliza kwenye nafasi zitakazowawezesha kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa mwaka wa nne sasa.

USAJILI: Simon Msuva aiangukia Yanga
Na Khatimu Naheka na Iman Makongoro,
Kwa ufupi
- Ukiacha Nonda Shaaban ‘Papii’, hakuna mchezaji mwingine aliyefanikiwa kung’ara au kuuzwa nje ya nchi akitokea Yanga.
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa
Yanga, Simon Msuva amereja nchini akitokea Afrika Kusini kufanya
majaribio ya soka la kulipwa na amewaangukia viongozi wake kutofanya
makosa ya kuzuia uhamisho wake.
Msuva mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
katikati ya wiki iliyopita alitoroka na kwenda Afrika Kusini kufanya
majaribio katika klabu ya Bidvetes Wits inayoshika nafasi ya tatu katika
msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ikiwa na pointi 52 juu ya Mamelodi
Sundowns 57 na vinara Kaizer Chiefs wenye pointi 69.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kuwasili
juzi, Msuva alisema amefanikiwa kuandika historia katika maisha yake ya
soka kwa kufanya majaribio katika klabu ya Wits na sasa anasubiri majibu
ya majaribio hayo kabla ya kuanza mchakato wa uhamisho.
Msuva ambaye amefunga mabao 17 katika Ligi Kuu
msimu huu alisema anauomba uongozi wa klabu yake chini ya mwenyekiti
Yusuf Manji kutoweka ugumu katika uhamisho huo badala yake wafanye
taratibu nyepesi ili aweze kucheza soka nje ya Tanzania.
“Unajua haya ni maisha na hii ni nafasi yangu ya
pekee niliyopata, nashukuru kila kitu kilienda sawa, ombi langu kwa
uongozi ni kunisaidia nikamilishe ndoto yangu,”alisema Msuva.
“Uongozi ningeuomba endapo hawa jamaa (Wits)
watakuja kuanza mchakato wa usajili wasiwe na tamaa ya fedha kwa kutaja
kiasi kikubwa ambacho kitakwamisha uhamisho wangu.”
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha
alilithibitishia gazeti hili jana kuwa hawana mpango wa kumuwekea
vikwazo Msuva huku akibainisha kuwa wanachohitaji ni taratibu zifuatwe
ingawa hadi jana mchana hakuna kiongozi wala wakala wa klabu ya Bidvest
aliyewafuata.
“Kama kweli wana nia na Msuva, tuko tayari
kumwachia akatafute maisha mengine ya soka nje ya nchi, madai kuwa tuna
mpango wa kuweka dau kubwa ili kumkomoa si kweli, tutaweka dau ambalo
kwetu tunaona ndilo linafaa kumuuza Msuva,” alisema katibu huyo.
“Kama timu inayomtaka itashindwa dau letu basi
haimuhitaji, mbona kuna wachezaji wanauzwa hadi dola milioni moja, dola
laki saba na kuendelea? Hivyo Msuva ‘akithitibisha’ anaweza, fedha
tunayoitaka haitakuwa ya kushtua,” alisema Tiboroha bila kubainisha ni
kiasi gani.
Tiboroha alisema walitarajia kukutana na Msuva jana jioni ili kujua hatma yake endapo anaondoka Yanga au la.
Yanga imekuwa na tabia ya kuwazuia wachezaji wake
wanapotakiwa na klabu mbalimbali nje ya nchi, ilishafanya hivyo kwa
Jerryson Tegete na Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima.
Mwaka 2009, Ngassa alitakiwa bila ya kufanya
majaribio katika klabu ya Lov-Ham ya Norway kwa gharama ya Dola za
Marekani 50,000, lakini Yanga walisema klabu yao ni kubwa ambayo haina
shida na ina uwezo wa kuwalea wachezaji wake na ndiyo maana haipo tayari
kuwauza nyota wake kwa bei rahisi na pengine wangelipwa zaidi ya Dola
za Marekani 100,000 wangeweza kumwachia.(Mwananchi)
New S. African Democratic Alliance Leader Rejects ‘Token Black' Label
Newly-elected
Democratic Alliance (DA) party leader Mmusi Maimane, delivers his
victory speech May 10, 2015, in Port Elizabeth, South Africa.
May 11, 2015 12:15 PM
JOHANNESBURG— South Africa's main
opposition party, the Democratic Alliance (DA), has elected its first
black leader. Mmusi Maimane takes over from Helen Zille, who has been
at the helm of the party for eight years.
At 34 years of age, the charismatic politician known for his sharp oratory skills and slick campaigns is often dubbed the “Obama of Soweto."
Mmusi Maimane pushes away such comparisons, but observers say his appointment as the new leader DA party could help shift a political landscape that currently tilts heavily in favor of the ruling African National Congress (ANC) party.
The eldest of four siblings, Maimane was born in Krugersdorp and brought up in Soweto - a township on the edges of Johannesburg that became the political epicenter of the anti-apartheid struggle.
Maimane joined the DA in 2010. He quickly rose through the ranks to become the party’s national spokesman in 2011. Last year, he lost his bid to lead the provincial government of South Africa's wealthiest province, Gauteng.
As the party's parliamentary leader, he accused President Jacob Zuma of being a “thief” during a heated parliamentary debate in March. His colleagues say he has a good sense of humor but is an “absolute perfectionist."
On May 10, Maimane became the DA’s first black party leader during a party conference with 88.9 percent of the vote.
Despite the DA’s growth in the last few elections – 12.4 percent of the vote in 2004, 16.7 percent in 2009 and 22.2 percent in 2014 – the party is still considered “too white” to threaten the supremacy of the ruling ANC, says political analyst Nic Borain.
Electing Maimane as party leader is one of several steps the DA is taking to enable it to dig into the ANC’s core constituency, Borain says.
“Mmusi is very specifically tailored. He was chosen and his rise was so quick because he fits exactly the profile the DA wants. His appointment is a necessary but not sufficient condition for the DA to break out of its racial confines. Mmusi is the transitional object,” says Borain.
Maimane has a bachelor's degree in psychology from the University of South Africa and a master’s degree in theology from Bangor University in the United Kingdom.
Before getting into politics, the gangly, eloquent leader - included in GQ magazine's 2014 list of best-dressed men - lectured at a business school in Johannesburg. A devout Christian, he is a preacher at the charismatic Discovery Church in Randburg.
Borain says it’s Maimane’s “popular appeal” the DA is hoping to capitalize on.
“Electing a leader who is a preacher in charismatic churches is a particular kind of appeal which the DA historically shied away from – a popular appeal. I think it is part of the compromises the DA is prepared to make with its principled ideology historically to reach new voters, new young black voters,” says Borain.
The ANC has said that he is too young and that his rapid elevation is a symptom of racial tokenism – a label flatly rejected by Maimane’s colleague and shadow minister for public enterprises, Natasha Michaels.
“Calling Mmusi a token black is an absolute insult. I think the fact that he received the overwhelming landslide victory that he did proves that black, white, colored, Indian, Asian – we all agreed that he was the man for the job and he was the man to take us forward,” said Michaels. “The energy of his age is going to be a huge advantage. He brings a certain dynamic to parliament that is desperately needed because we are a very young country," added Michaels.(source VOICE OF AMERICA)

Ijumaa, 8 Mei 2015
SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO TAYARI IMESAINIWA NA RAIS
Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya
mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza kutumika rasmi
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema hayo leo wakati akizungumzia masuala mbali mbali yanayohusu sheria hiyo ambayo kupitishwa kwake kumesababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau kuwa itaminya uhuru wa habari, kuingilia faragha pamoja na uhuru wa watu kuwasiliana.

Huu ni uchambuzi kidogo kuhusu baadhi ya vipengele vilivyozua utata katika muswada uliokuwa umetolewa
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).
2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).
3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; (Mfano: mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!)
4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?
5 Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. (Mfano: unapofuta ‘status’ zako za WhatsApp, unaweza shitakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.)
6. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.
7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha(SOURCE:East Africa Television (EATV)

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)