ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 15 Mei 2016

MAGAZETINI:#Watumishi 10,870 wa sekta ya afya kuajiriwa

OFISI ya Rais, Utumishi na Utawala Bora imesema katika mwaka ujao wa fedha 2016/17 inatarajia kuajiri watumishi wa sekta ya afya 10,870 kwa ajili ya kupunguza pengo la uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.
Hayo yalisemwa bungeni Dodoma juzi na Waziri wa wizara hiyo, Angella Kairuki, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2016/17.
“Nimesikia katika michango mingi wabunge wamezungumzia sana tatizo la uhaba wa watumishi wa sekta ya afya. Waheshimiwa wabunge katika mwaka ujao wa fedha sekta ya afya wataajiriwa watumishi 10,870,” alisema Kairuki.
Alisema muda wowote kuanzia sasa ndani ya mwezi huu, vibali vya ajira hizo vitatoka na wizara ya afya, itaendelea kuwapangia watumishi sehemu zao za kazi. Kairuki alisema katika mgawanyo huo wa watumishi 10,870, watumishi 3,147 ni wa kada mbalimbali 10 zinazohusu masuala ya mbalimbali ya utabibu, wauguzi 3,985 na kada nyingine za mama cheza, wataalamu wa viungo na famasia.
Alisema katika kuangalia namna serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika utoaji wa ajira kwenye sekta afya, ndani ya miaka mitano serikali ilitoa vibali vya ajira 52,947 na kati ya vibali hivyo walioweza kuajiriwa ni wataalamu 38,047.
Kairuki alisema kati ya waajiriwa hao, ambao hawakuripoti ni 14,860 ; na asilimia 71.93 ndio walioweza kuripoti. “Ukiangalia takwimu za mwaka jana 2014/15 pamoja kwamba ikama zimejazwa na halmashauri zetu, ziko kada zaidi ya 12 zenye wataalamu 335 hazikuweza kupata watu kabisa, ukiangalia kada hizo hata mafunzo yake hapa nchini hayatolewi, kwa mfano wataalamu kutoka kada ya biomedical engineers na wengine wengi,” alisema.
Aidha alisema katika mwaka 2014/15, Serikali ilitoa kibali cha watumishi 8,345, lakini katika soko la ajira kulikuwa na ukosefu wa wataalamu katika soko hilo 4,467. Alitoa mfano wahitimu wa mwaka 2015/16 ni wataalamu 10,000 wakati Serikali imetoa kibali cha ajira cha wataalamu 10,870.
Alisema katika mwaka wa fedha 2010/11, Serikali katika sekta ya afya ilianza na watumishi 7,300, lakini katika mwaka ujao wa fedha idadi hiyo itaongezeka na kufikia 10,870. Kairuki alisema serikali itaangalia namna ya kuwapanga watumishi hao kwa kuzingatia maeneo

MAGAZETINI:#Uingereza kusaidia usambazaji umeme

MIEZI michache baada ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) kujitoa kusaidia Tanzania katika usambazaji wa umeme vijijini, Serikali ya Uingereza kupitia taasisi yake ya Energy Africa Initiative, imetangaza utayari wa kutoa msaada huo.
Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ameeleza utayari huo mwishoni mwa wiki, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliye nchini humo kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani. Katika mazungumzo hayo, Greening alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake wa kupeleka umeme vijijini.
“Tuko tayari kuwasaidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema. Pia Waziri huyo wa Uingereza, alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu wa kushiriki mkutano huo, kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali ya Rais Magufuli.
Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeionesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda. Nguvu mpya Rea Hatua hiyo ya Uingereza, imekuja wiki moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Alhamisi wiki ijayo, ambayo mjadala wake utafanyika kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa, unatarajiwa kuibua hoja ya kufutwa kwa msaada huo wa MCC wa Dola za Marekani milioni 472, uliokuwa utumike kusambaza umeme vijijini.
Mbali na mjadala huo ambao unatarajiwa kung’ang’aniwa na Kambi ya Upinzani Bungeni, hatua hiyo ya Uingereza itaongeza nguvu katika jitihada za Serikali zilizokwishaanza kwa mafanikio za kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika. Taarifa za Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) zinaonesha kuwa, pamoja na MCC kujitoa Machi mwaka huu katika usambazaji umeme, Serikali katika Bajeti ya 2015/ 2016 inayoisha Juni mwaka huu, ilikuwa imeshatenga Sh bilioni 950 kwa ajili ya mradi wa Rea Awamu ya Pili.
Mradi huo wenye lengo la kufikisha umeme kwa vijiji 2,500 na kuunganishia nishati hiyo wateja 250,000 nchi nzima, unatarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu na kupisha kuanza kwa Rea Awamu ya Tatu, ambayo itaanza Julai mosi na kumalizika baada ya miaka miwili. Jitihada zote hizo, lengo lake ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015-2020, ambayo inataka hadi ifikapo mwaka 2020, wananchi waliounganishwa na umeme wafikie asilimia 60 na kiwango cha uzalishaji kifike megawati 4,915.
Mbali na malengo ya Ilani hiyo, jitihada hizo pia zitachangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotaka Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambayo imeweka lengo la usambazaji umeme liwe asilimia 50 mwaka huo mwaka 2025 na asilimia 70 mwaka 2033.
Tayari Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameshaelezea nia ya Serikali kutaka sekta ya nishati itoe mchango mkubwa kufikia uchumi huo wa kati, kwa kuwa rasilimali za kufikia lengo hilo kupitia nishati zipo na kinachotakiwa ni dhamira na kasi ya kutekeleza.
Katika kusisitiza kasi na dhamira hiyo ya Serikali, Waziri huyo amekuwa akielezea mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa dira hiyo, iliyotaka ifikapo mwaka 2015 uunganishaji umeme uwe umefikia asilimia 30. Lakini, kutokana na utekelezaji madhubuti wa dira hiyo, kiwango hicho kilivukwa lengo na kufikia asilimia 40 mwaka 2015.
JPM na Marekani Mbali na msaada huo wa Uingereza katika kusambaza umeme vijijini, Serikali ya Marekani pia imeelezea kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, hatua iliyoanza kuvutia wawekezaji wa nchi hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Sarah Sewall, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu Majaliwa nchini Uingereza katika mkutano huo wa kimataifa, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa.
Alisisitiza kuwa kampuni nyingi za Marekani, zimeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania. “Ninaamini uwekezaji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu. Tunampongeza Rais Dk Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.
Majaliwa ashukuru Akizungumza katika kikao chake na Waziri Sewall, Waziri Mkuu Majaliwa alimsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza Wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini.
Alimhakikishia kuwa Watanzania wamekuwa wakijifunza teknolojia mpya na za kisasa. Kuhusu mafanikio katika mapambano na rushwa, Majaliwa alisema mkutano huo wa kimataifa, uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani, ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo.
Akizungumza na mawaziri hao, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba viongozi wa Serikali wa Awamu ya Tano, wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu, linalotokana na janga la rushwa na wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa, ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongoni mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa nini kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hiyo, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe ama kupokelewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.
“Serikali inachukua hatua za kiutawala na kisheria, kama vile kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.

MAGAZETINI:#.DC Kinondoni akemea vigogo wa sukari wanaompigia simu

Imeandikwa na Katuma Masamba MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amefichua kuwa amekuwa akipigiwa simu na baadhi ya wafanyabiashara vigogo wenye nia ya kutaka kupunguza makali ya operesheni inayofanywa na wilaya yake dhidi ya waficha sukari.
Kwamba simu hizo amekuwa akipigiwa hadi usiku wa manane na huku wengine wakimtumia ujumbe mfupi wa simu wa maandishi (SMS). Amekemea wafanyabiashara hao na kutaka waache mara moja mchezo huo, kwani vyombo vya dola vinaendelea kuwafuatilia.
Hapi alisema hayo jana wakati akizungumzia suala la Uadilifu kwenye Mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wanaotokana na shirikisho hilo.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba amekuwa hapokei simu hizo na SMS hizo za wafanyabiashara wakubwa kutokana na sababu mbalimbali. “Sababu ya kwanza sina sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao, kuonesha nipo pamoja nao.
“Wakati mwingine mpaka usiku wa manane wanapiga simu na kutuma meseji na wengine wanajitambulisha. Lakini huwa namuonyesha mke wangu na kumwambia sina sababu ya kuzipokea, kwani naweza nikapokea lakini katika mazungumzo yetu nikasema neno ‘sawa’, kisha neno hilo linaweza kusambazwa katika mitandao kuonyesha kwamba nia yetu ni moja ya kuficha sukari”, alisema Hapi.
Alisema hao wafanyabiashara wanaoficha sukari, wanaleta madhara makubwa kwa jamii na uchumi wa nchi, kama vile kuua viwanda vya sukari nchini. Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiweka ‘oda’ katika viwanda vya sukari kuchukua bidhaa hiyo, lakini hawaendi kuichukua kwa madai ya kwenda kuichukua siku za baadaye, lengo likiwa kuificha. Hapi aliwaomba wakazi wa wilaya ya Kinondoni, kuendelea kuisaidia serikali kufichua watu wote walioficha sukari.

Magazeti ya Leo jumapili ya tarehe 15may 2016 Kwa hisani ya Airtel jipimie yatosha




Furahia nasi tunakutakia jumapili njema na yenye fanaka tele .










 Endelea kusoma magaazeti yetu kila siku





Jumamosi, 14 Mei 2016

Wamiliki wa Blogs Tanzania ndani ya bunge Kwa Mwaliko wa Waziri Nape Nnauye

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgafp0Vztm3iFYGuUkrTwdbfUE__2jE9_l6A_rSJ511uicNWaaxDj3t4_d3m-yae5wusmNO-XINyorWH3kM6eqTuJfY3BW_Ql6S8cILVXlXd5aYnnj2nxa2CcMFywZSKGUHME251JTSwTI/s640/01.JPG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wamiliki wa Blogs (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia Wambura.  
 
Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhU6tb3c90xAE43ovHZT2eQ6KfAKa4JMU9SIaeuFsvSiMuzK58LgoTlFr6BhARMyLxNuGQkCD59DjAE-jwmlx9IDg5_GPhwDKJLf9b1WZa2D-ebvET-Spnk2sGmQR5Izro7R8PF-EN52go/s640/IMG_1100.JPG 
Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYrUW_AQMGACBg62PGeELJHeX-giqpzHprC2yoJmZI39StG5GTMOlt5Tkief_PBbwIvSMLNSj6zade3d7naT8NQHUCzP4d31aGy4vtc-ws2jleQfxbzqGRriufqeqJGPSmHroOmT2Q4qw/s640/IMG_1106.JPG  

Wanataaluma wa chuo kikuu kishiriki cha Dar Es Salaam(DUCE) wachangia damu

Na Kilangi stanley
Baadhi ya viongozi wa chuo kikuu cha DUCE wakijiandaa kuchangia damu





Tazama video ya mahojiano tukiwa na wachangiaji wa damu huko DUCaE.   


MAGAZETINI:#Azam yapata makocha Wahispania

KLABU ya soka ya Azam FC ya Dar es Salaam imepata makocha wawili kutoka klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania. Makocha hao Zebensul Hernandez Rodriguez ambaye atakuwa Kocha Mkuu na Jonas Garcia Luis kocha wa viungo, waliwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana na kupokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saada Kawemba.
Kwa mujibu wa Kawemba watafanya mazungumzo na makocha hao na kama watakubaliana watawachukua ili wainoe timu yao. Kocha wa sasa wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu wa ligi.
“Wamekuja kwa ajili ya mazungumzo, tukikubaliana tutawachukua kwa ajili ya timu yetu,” alisema Kawemba. Kwa upande wake Rodriguez alisema amefurahi kuja nchini kwani anaamini kuna vipaji vya soka kwa jinsi walivyomuona mchezaji Farid Mussa wa Azam ambaye anafanya majaribio katika timu yao.
Farid Mussa ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefuzu majaribio katika klabu hiyo iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania na kilichobaki ni mazungumzo baina ya Azam na klabu hiyo kuhusu mauzo ya mchezaji huyo.