Imeandikwa na Mwandishi Wetu
YANGA inaleta heshima kwa Watanzania. Pengine ndivyo unavyoweza
kuzungumzia matokeo ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF
CC), ambapo Yanga imeingia hatua ya makundi ya mashindano hayo.
Imevuka licha ya kufungwa 1-0 na wenyeji wao, Sagrada Esperanca ya Angola katika mchezo uliofanyika katika mji wa Dundo.
Bao pekee la Waangola hao liliwekwa kimiani na mshambuliaji mkongwe
mwenye umri wa miaka 37, lakini mahiri, Arsenio Sebastiao Cabungula
`Love’ katika kipindi cha kwanza.
Yanga imenufaika na ushindi wa 2-0 ilioupata Mei 7 jijini Dar es
Salaam kutokana na mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony, na hivyo
kufuzu kwa jumla ya mabao 2-1.
Katika mchezo wa jana, Yanga ilicheza kwa nguvu zaidi karibu muda
mwingi wa mchezo, ambapo washambuliaji wake wakiongozwa na Donald Ngoma
walifika mara kadhaa langoni mwa wapinzani wao, lakini umaliziaji
ulikuwa mbaya.
Dakika ya 90, kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ alipangua penalti
iliyotolewa baada ya beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumchezea madhambi
mshambuliaji wa Sagrada.
Kwa kuingia hatua ya makundi Yanga imeandika historia mpya katika
soka nchini kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kufuzu hatua hiyo katika
mashindano hayo, lakini ni mara ya pili kufuzu hatua ya makundi kwa
mashindano makubwa Afrika baada ya kufanya hivyo mwaka 1998 katika Ligi
ya Mabingwa Afrika.
Simba ya Dar es Salaam nayo ilifuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa
Afrika mwaka 2003 kwa kuitoa na kuivua ubingwa Zamalek ya Misri. Yanga
imeangukia Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC), baada ya
kutolewa na Al Ahly ya Misri hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika
kwa jumla ya mabao 3-2, ililazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na
kufungwa mabao 2-1 Alexandria, Misri.
Ilizitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa mabao 3-0, ikishinda 1-0
ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao
3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa
Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1
ugenini na kushinda 2-0 nyumbani.
Katika raundi ya kwanza waliitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa mabao 2-1,
ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya
16 Bora, ambako waliitoa V.Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1
wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
Pamoja na Yanga katika hatua hii, timu nyingine zilizoingia na
zimeshaanza kucheza mechi za mtoano – mbili, nyumbani na ugenini kabla
ya nne kufuzu kwa hatua ya makundi zikichanganywa na zilizokuwamo ni
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Al-Merreikh ya Sudan.
Nyingine ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC);
Etoile du Sahel ya Tunisia; Stade Malien ya Mali; Al-Ahli Tripoli ya
Libya; MO Bejaia ya Algeria.
Kutokana na kusonga mbele huko na kuingia katika makundi, kama Yanga
ikishika nafasi ya nne itavuna dola 150,000 (Sh milioni 315) huku
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakilamba dola 15,000 (Sh milioni
31.5).
Wakishika nafasi ya tatu kwenye kundi wanachukua dola 239,000 (sh milioni 501) na TFF kupata dola 20,000 (Sh milioni 42).
Yanga hawa ambao kocha msaidizi ni Juma Mwambusi waliyemchukua Mbeya
City baada ya Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ kwenda Taifa Stars
wakishika nafasi ya pili kwenye kundi lao watapata dola 239,000 na
shirikisho la Rais Jamal Malinzi yaani TFF linapata dola 25,000 (Sh
milioni 52.5).
Yanga wakifika fainali; hata wasipolitwaa kombe basi watakuwa tayari
mezani mwao wana dola 432,000 (Karibu Sh milioni 900) na TFF kupata dola
30,000 (Sh milioni 62) na ikiwa wanafunika bara zima kama Mlima
Kilimanjaro ulivyo paa la Afrika, zao ni dola 625,000 (zaidi ya Sh
bilioni 1.3 za Tanzania) na TFF wanalamba dola 35,000 (zaidi ya Sh
milioni 70).
Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/
Deus Kaseke, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Kevin Yondan na Haruna
Niyonzima.
TANGAZO
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE
Mahali:
Ilula madizini katika majengo ya kanisa katoriki kigango cha madizini
karibu na soko la TASAF.
Inawatangazia
kuwa inaendelea na utoaji wa huduma (tuition) kuanzia kidato cha kwanza
mpaka cha sita: tuition hii ni mahususi kwaajili ya likizo ya
mwezi wa sita itaanza usajiri wake kuanzia tarehe 30/05/2016.
Ada ni
shilingi Elfu kumi(10,000) kwa muda wote wa likizo
- kwa wanafunzi wa kidato cha
nne(form 4) tutafanya
solving ya past paper na maswali mbalimbali
pia mwanafunzi
atapewa peni bure na notes zilizo andaliwa na walimu mahili mara tu baada ya kufanya usajiri. Nyote mnakaribisha kwa mawasiliano
piga simu no +255769694963 au +255784428256.