ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 18 Mei 2015

Mwalimu wa shule ya msingi Isagwa ajinyonga-kilolo-Iringa


 Mwalimu wa shule ya msingi Isagwa ajinyonga huko wilaya ya kilolo mkoani iringa akiwa chumbani kwake, huku akishangaza wengi siku hiyo ilikuwa ndio kikao cha mwisho cha Harusi yake, pia ameandika ujumbe unaosema nimechoka kutishiw, Mwalim huyo anayejulikana kwa jina la kisoma

Jumamosi, 16 Mei 2015

MATOKEO FORM TWO 2014 YALIYOKUWA YAMEZUIWA SABABU YA ADA YA MTIHANI


MATOKEO FTSEE 2014 YALIYOKUWA YAMEZUIWA KWA SABABU YA ADA YA MTIHANI  Bofya Hapa

SHULE ZA KIDATO CHA TANO ZIONGEZWE-RAIS

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza Wakuu wa Mikoa na Maofisa Elimu wote nchini, kuanza ujenzi wa shule maalumu za kidato cha tano na sita kwa kila kata na wakishindwa, katika shule za sekondari za kata, wachague baadhi na kujenga madarasa ya vidato hivyo.

Alitoa agizo hilo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, yaliyoadhimishwa kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na kuwakumbusha kuwa kati ya wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha tano mwaka huu, ni asilimia 75 tu walioendelea na masomo hayo.

“Wakuu wa mikoa na maofisa elimu mliopo hapa naagiza na hili ni kwa nchi nzima, tuanze utaratibu wa kuwa na shule za kidato cha tano na sita za kata. Mnaweza kujenga shule mpya, au mchague baadhi ya sekondari za kata ziwe na kidato cha tano na sita,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kusema si vyema kuwaacha mtaani asilimia 25 wenye sifa ya kuingia kidato cha tano.

Alisema bila kuchukua hatua hiyo, Tanzania inaweza kurudi katika hali ya elimu aliyoikuta ambapo wanafunzi wenye sifa ya kuendelea na masomo, waliachwa kutokana na ufinyu wa nafasi za kuendelea na elimu.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakati alipokuwa akiingia madarakani, alikuta asilimia sita tu ya wanafunzi waliokuwa wamefanya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, ndio waliokuwa wakichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.

“Leo kila anayefaulu darasa la saba, anakwenda sekondari… tukisema leo mwanafunzi amefeli darasa la saba amefeli kweli tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichaguliwa,” alisema Rais Kikwete.

Tanzania ilipotoka Rais Kikwete alielezea sababu ya Serikali inayomaliza muda wake kuwekeza zaidi katika elimu, kiasi kwamba bajeti ya elimu katika Mwaka wa Fedha unaoisha kuwa kubwa kuliko ya sekta zingine, inayofikia Sh trilioni 3.4 kutoka Sh bilioni 600 iliyokuwepo mwaka 2005.

Sababu ya kwanza Rais Kikwete alisema, waliona kuwa kuwekeza katika elimu ndio kuwekeza katika taifa na Serikali isingechukua uamuzi huo, Watanzania hawataweza kutawala mazingira yao na kutumia vizuri rasilimali zao.

Pili alisema alipoingia madarakani, alikuta Tanzania yenye watu wengi zaidi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iko nyuma ikilinganishwa na Kenya na Uganda, kwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma shule za sekondari na vyuo.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, mwaka 2005 wanafunzi waliokuwa wakisoma sekondari ni zaidi ya 500,000, wakati nchini Uganda waliokuwa wakisoma sekondari walikuwa zaidi ya 700,000 na Kenya zaidi ya 900,000.

Kwa upande wa vyuo vikuu, Tanzania ilikuwa na wanafunzi 40,000 tu wakati Uganda ilikuwa na wanafunzi 124,000 na Kenya 180,000.

“Kuwa nyuma katika kutoa fursa ya elimu ikilinganishwa na wenzetu ilikuwa inaweka nchi yetu katika mazingira mabaya katika ushindani wa soko la ajira la Afrika Mashariki,” alisema Rais Kikwete.

Mbali na mazingira mabaya katika ushindani wa soko la Afrika Mashariki, Rais Kikwete alisema Watanzania nao walifikia hatua ya kuamua kupeleka watoto wao kwenda kusoma Kenya na Uganda.

Hatua zilizochukuliwa, Rais Kikwete alisema Serikali kwa kushirikiana na wananchi, waliamua kujenga shule za sekondari za kata, ambapo wananchi walihamasishwa, wakahamasika wakajenga shule mpaka Mkurugenzi mmoja wa elimu, akahofia kukosa walimu wa kupeleka katika shule hizo.

“Tulihimiza wadau wengine wajenge vyuo vya elimu ya juu na kuamua mikopo ya elimu ya juu itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vyote,” alisema Rais Kikwete.

Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania ina wanafunzi 1,800,000 wanaosoma sekondari na imeshaipita Uganda yenye wanafunzi 1,700,000 wanaosoma elimu ya sekondari, lakini imezidiwa na Kenya ambayo ina wanafunzi 2,100,000.

Hata hivyo alisema ni rahisi kuipita Kenya kwa hilo pengo la wanafunzi 300,000, kwa kuwa shule za sekondari zilizopo zina nafasi ya kuongeza wanafunzi milioni mbili zaidi.


“Hapa lazima tuwafukuzie Wakenya, lazima tuwakute na kuwapita na huu ni ushindani mzuri kwa kuwa ni ushindani wa maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema vyuo vikuu vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi kufikia 52 na idadi ya wanafunzi walio katika vyuo vikuu ilitoka 40,719 hadi kufikia 200,956.


Chanzo:
Habari Leo

Jumatano, 13 Mei 2015

NEC sasa yaanza kugawa majimbo


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza rasmi mchakato wa kugawa majimbo ya uchaguzi nchini ambapo inatarajia kuanza uchunguzi wa mipaka ya majimbo hayo hivi karibuni, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Aidha, tume hiyo imesisitiza kuwa uchaguzi mkuu lazima ufanyike Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa Katiba, na kufafanua kuwa kwa mujibu wa ratiba ya uandikishaji wapigakura kwenye daftari la wapigakura, uandikishaji huo unatarajiwa kukamilika Julai mwishoni au Agosti mwanzoni mwaka huu.
Akifungua mkutano baina ya tume hiyo na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Damian Lubuva, alisema uchaguzi na mgawanyo huo wa majimbo unafanyika chini ya Katiba ya sasa ya mwaka 1977.
“Tume inapenda kuwahakikishia kuwa ugawaji huu wa majimbo utakamilika kwa wakati na wananchi watajulishwa ili vyama vya siasa viweze kuteua wagombea katika majimbo hayo,” alisisitiza Jaji Lubuva.
Alisema kwa sasa utaratibu wa kuandikisha wananchi kwenye daftari hilo la kudumu la wapigakura unaendelea vizuri na Serikali imeshatoa fedha zote za ununuzi wa vifaa vya kuandikishia zikiwemo BVR kits.
Alisema hadi sasa jumla ya BVR 4,800 zimeshawasili na zinaendelea kutumika katika uandikishiaji na Mei 20, mwaka huu BVR kits 1,600 zinatarajiwa kuwasili na Mei 29, mwaka huu pia BVR 1,520 zitawasili kwa ajili ya uandikishaji.
Alisema ratiba ya uandikishaji tayari imeshatoka na kwamba kwa sasa tume hiyo inaendelea kuandikisha ambapo Mei 19, mwaka huu tume hiyo itaandikisha wananchi wa mikoa ya Singida, Tabora, Igoma na Kagera na kufuatiwa na mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu.
Aidha pia ratiba hiyo inaonesha baada ya mikoa hiyo, uandikishaji utaendelea katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Zanzibar na kumalizikia mkoani Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alitaja vigezo vitakavyotumika kugawa jimbo kuwa ni mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu ambao utazingatia takwimu za idadi ya watu kutoka Ofisi ya Takwimu (NBS) na idadi ya majimbo ambayo kwa sasa ni 239.
“Kwa mujibu wa makadirio ya ofisi ya takwimu Watanzania wote Tanzania bara wamefikia milioni 47.1, kwa upande wa majimbo ya mjini yana watu takribani milioni 10 na vijijini watu milioni 37,” alisema Malaba.
Alisema kutokana na takwimu hizo, mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu kwa majimbo ya mjini utazingatia watu 325,000 na kwa upande wa majimbo ya vijijini wastani utakuwa ni watu 250,000, hivyo majimbo yatakayogawanywa ni yale yenye idadi ya watu zaidi ya mgawanyo huo.
Alitaja vigezo kingine kuwa ni upatikanaji wa mawasiliano kama vile barabara, simu na vyombo vya habari, hali ya kijiografia kwa mfano maeneo ya mlimani, visiwani au mabondeni ni kigezo kingine cha mgawanyo wa jimbo pamoja na hali ya uchumi.
Kigezo kingine ni ukubwa wa eneo la jimbo husika, mipaka ya kiutawala, jimbo moja lisiwe ndani ya wilaya au halmashauri mbili ambapo endapo kwa sasa zipo wilaya au halmashauri zilizogawanywa, tayari zimeshatoa mgawanyo wa majimbo.
Aidha kigezo kingine ni kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili, mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo, mazingira ya muungano, uwezo wa ukumbi wa Bunge na viti maalum vya wanawake ambavyo kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya mwaka 1977 imetenga zaidi ya asilimia 30 ya viti vya ubunge kwa ajili ya wanawake.
Alisema tume hiyo inatarajia kukutana na wadau na kujadiliana juu ya vigezo na utaratibu utakaotumika kuchunguza mipaka na kugawa majimbo, kupokea maombi na mapendekezo ya kugawa, kurekebisha mipaka au kubadili majina ya majimbo kutoka kwa wadau na kuainisha maombi hayo.
Malaba alisema tume hiyo imeweka utaratibu wa wadau kuwasilisha maombi ya kurekebisha mipaka na kugawa majimbo au kubadili majina ya majimbo ambayo yatawasilishwa kwa mkurugenzi wa halmashauri husika na kujadiliwa na vikao rasmi.
“Mkurugenzi atawasilisha maombi au mapendekezo hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye atayawasilisha katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ili kupata maoni zaidi na mwisho Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha maoni hayo kwa NEC,” alisisitiza.
Kwa upande wake Kamishna wa Tume, Profesa Amone Chaligha, alisema tume hiyo inatarajia kutoa ratiba kamili ya ugawaji wa majimbio hayo na matangazo yake kesho ili suala hilo, litekelezwe mapema iwezekanavyo.
Nao wawakilishi wa vyama vya siasa, akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na Mwenyekiti wa chama cha NLD, waliitaka tume hiyo, kuweka wazi ratiba zote zinazoendana na mchakato wa uchaguzi, ili vyama hivyo vijiandae vyema.(HABARI LEO)

welcome small city ILULA- HOME OF HOSPITALITY


Population of Ilula:

29 193 people

Latitude of Ilula:

-7,6833 (740'59.988"S)

Longitude of Ilula:

36,0333 (361'59.880"E)

Altitude of Ilula:

1 505 m

Article: Tanzania

Biggest cities: Tanzania

Photos, pictures: Tanzania

All cities: Tanzania

The biggest cities of the World

GMT time in Ilula:

+3 hours

Distance from city Ilula to 25 biggest cities of country: Tanzania

Distance (Km)
 Ilula - Dar Es Salaam  372 km
 Ilula - Unguja Ukuu  398 km
 Ilula - Mwanza  671 km
 Ilula - Zanzibar  387 km
 Ilula - Arusha  485 km
 Ilula - Mbeya  315 km
 Ilula - Morogoro  204 km
 Ilula - Tanga  447 km
 Ilula - Dodoma  170 km
 Ilula - Kigoma  774 km
 Ilula - Moshi  503 km
 Ilula - Moschi  503 km
 Ilula - Tabora  464 km
 Ilula - Songea  336 km
 Ilula - Musoma  731 km
 Ilula - Mazama  731 km
 Ilula - Iringa  38 km
 Ilula - Katumba  317 km
 Ilula - Shinyanga  531 km
 Ilula - Mtwara  539 km
 Ilula - Ushirombo  648 km
 Ilula - Kilossa  141 km
 Ilula - Sumbawanga  488 km
 Ilula - Bagamoyo  346 km
 Ilula - Bagamojo  346 km

Distance from city: Ilula to Top 10 cities of the world

Distance (Km)
 Ilula - Berlin  6 992 km
 Ilula - London  7 385 km
 Ilula - Los Angeles  16 065 km
 Ilula - Moscow  6 973 km
 Ilula - New York  12 262 km
 Ilula - Paris  7 034 km
 Ilula - Peking  9 691 km
 Ilula - Rio De Janeiro  8 565 km
 Ilula - Sydney  11 806 km
 Ilula - Tokyo  11 679 km
 Ilula - Prague  6 761 km

Jumatatu, 11 Mei 2015

Simba yaridhika Kagame na nafasi ya tatu


11 May2015
KOCHA Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema anashukuru kumaliza ligi katika nafasi ya tatu na sasa anasubiri hatima yake.
Simba ilimaliza ligi juzi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kumaliza ya tatu ikiwa na pointi 47.
Kopunovic alianza kuiongoza Simba mwishoni mwa raundi ya kwanza akichukua mikoba ya Patrick Phiri aliyetupiwa virago baada ya timu kutopata matokeo mazuri.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kopunovic alisema ligi ilikuwa na changamoto nyingi na kumaliza nafasi ya tatu ni jambo la kushukuru.
“Halikuwa lengo letu, wote tulitaka kutwaa nafasi kubwa zaidi, lakini ligi ilikuwa na changamoto nyingi, nitakabidhi ripoti yangu kwa uongozi, hapo ndipo utajua hatima yangu,” alisema kocha huyo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba.
Akilizungumzia hilo, msemaji wa Simba Haji Manara alisema wanachokisubiri ni kuona ripoti ya kocha huyo kabla ya kufanya uamuzi mwingine.
“Watu wana papara ya kutaka kujua nini kitafuata, tumeshiriki ligi kama timu nyingine na yaliyotokea yametokea, kiutaratibu tunasubiri ripoti ya kocha ndipo mambo mengine yafuate kama kusajili ama la,” alisema.
“Tunataka tuwe na uhakika wa nini tunataka kufanya, kama mabadiliko ni yapi, yote hayo tunayafanya kwa muongozo wa ripoti ya kocha,” alisema Manara.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema, Simba imepania kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kumaliza kwenye nafasi zitakazowawezesha kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa mwaka wa nne sasa.

USAJILI: Simon Msuva aiangukia Yanga

Msuva 
Na Khatimu Naheka na Iman Makongoro, 
Kwa ufupi
  • Ukiacha Nonda Shaaban ‘Papii’, hakuna mchezaji mwingine aliyefanikiwa kung’ara au kuuzwa nje ya nchi akitokea Yanga.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amereja nchini akitokea Afrika Kusini kufanya majaribio ya soka la kulipwa na amewaangukia viongozi wake kutofanya makosa ya kuzuia uhamisho wake.
Msuva mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, katikati ya wiki iliyopita alitoroka na kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvetes Wits inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ikiwa na pointi 52 juu ya Mamelodi Sundowns 57 na vinara Kaizer Chiefs wenye pointi 69.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kuwasili juzi, Msuva alisema amefanikiwa kuandika historia katika maisha yake ya soka kwa kufanya majaribio katika klabu ya Wits na sasa anasubiri majibu ya majaribio hayo kabla ya kuanza mchakato wa uhamisho.
Msuva ambaye amefunga mabao 17 katika Ligi Kuu msimu huu alisema anauomba uongozi wa klabu yake chini ya mwenyekiti Yusuf Manji kutoweka ugumu katika uhamisho huo badala yake wafanye taratibu nyepesi ili aweze kucheza soka nje ya Tanzania.
“Unajua haya ni maisha na hii ni nafasi yangu ya pekee niliyopata, nashukuru kila kitu kilienda sawa, ombi langu kwa uongozi ni kunisaidia nikamilishe ndoto yangu,”alisema Msuva.
“Uongozi ningeuomba endapo hawa jamaa (Wits) watakuja kuanza mchakato wa usajili wasiwe na tamaa ya fedha kwa kutaja kiasi kikubwa ambacho kitakwamisha uhamisho wangu.”
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha alilithibitishia gazeti hili jana kuwa  hawana mpango wa kumuwekea vikwazo Msuva huku akibainisha kuwa wanachohitaji ni taratibu zifuatwe ingawa hadi jana mchana hakuna kiongozi wala wakala wa klabu ya Bidvest aliyewafuata.
“Kama kweli wana nia na Msuva, tuko tayari kumwachia akatafute maisha mengine ya soka nje ya nchi, madai kuwa tuna mpango wa kuweka dau kubwa ili kumkomoa si kweli, tutaweka dau ambalo kwetu tunaona ndilo linafaa kumuuza Msuva,” alisema katibu huyo.
“Kama timu inayomtaka itashindwa dau letu basi haimuhitaji, mbona kuna wachezaji wanauzwa hadi dola milioni moja, dola laki saba na kuendelea? Hivyo Msuva ‘akithitibisha’ anaweza, fedha tunayoitaka haitakuwa ya kushtua,” alisema Tiboroha bila kubainisha ni kiasi gani.
Tiboroha alisema walitarajia kukutana na Msuva jana jioni ili kujua hatma yake endapo anaondoka Yanga au la.
Yanga imekuwa na tabia ya kuwazuia wachezaji wake wanapotakiwa na klabu mbalimbali nje ya nchi, ilishafanya hivyo kwa Jerryson Tegete na Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima.
Mwaka 2009, Ngassa alitakiwa bila ya kufanya majaribio katika  klabu ya Lov-Ham ya Norway kwa gharama ya Dola za Marekani 50,000, lakini Yanga walisema klabu yao ni kubwa ambayo haina shida na ina uwezo wa kuwalea wachezaji wake na ndiyo maana haipo tayari kuwauza nyota wake kwa bei rahisi na pengine wangelipwa zaidi ya Dola za Marekani 100,000 wangeweza kumwachia.(Mwananchi)