Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kuzingatia
mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua katika utendaji
wao zinafuata Sheria ,Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Mei 9, 2017 wakati
akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Majaliwa
alisema kuwa viongozi hao wanatakiwa kusimamia kikamilifu nidhamu
katika Utumishi wa Umma kwa sababu wenyewe ni kioo katika kuishi kwa
kuzingatia miiko ya Utumishi wa Umma.
Aidha,
viongozi hao wametakiwa kutoa kipaumbelea katika kufuatilia na
kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu na maji kwa kuwa ndizo
zinazogusa zaidi maisha ya wananchi.
Pia,
Majaliwa aliwaelekeza wasimamie na kuziba mianya yote ya upotevu wa
dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya na kudhibiti migogoro ya
wakulima na wafugaji pamoja na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira
katika maeneo yao.
Naye
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Suleiman Jafo alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuhakikisha viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika utendaji wao
wa kazi ili Serikali iweze kupata tija.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni