ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 30 Januari 2016

Simba, Yanga leo tena

DURU la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara linaanza leo wakati timu 12 zikiwemo za Yanga na Simba kushuka kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu. Hata hivyo, Azam FC inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, leo ilitakiwa kucheza na Prisons ya Mbeya, haitashuka dimbani kwa sababu inashiriki mashindano ya timu nne nchini Zambia.
Yanga wenyewe wako kileleni wakiwa na pointi 39 sawa na Azam FC, lakini wanaongoza kwa uwiano wa tofauti ya magoli, leo watakuwa wageni wa Coastal Union katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Katika mchezo wa raundi ya awali, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga watataka kudhihirisha kuwa hawakubahatisha kuifunga Coastal katika mchezo wa kwanza, huku Wagosi hao wa Kaya nao watataka kudhihirisha wao sio wanyonge mbele ya mabingwa hao watetezi.
Vijana hao wa Jangwani wakishinda leo watakuwa wamejikusanyia pointi 42 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kuiacha Azam FC ikibaki na pointi zake 39 katika nafasi ya pili.
Kwa upande wa Simba, wenyewe katika mchezo wa kwanza dhidi ya African Sports uliochezwa Mkwakwani, iliibuka na ushindi kiduchi wa bao 1-0, hivyo na leo itataka kuendeleza ubabe dhidi ya vijana hao wa Tanga.
Simba yenye pointi 33, inazihitaji sana pointi tatu kutoka kwa African Sports ili angalau izidi kujisogeza katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam katika mbio hizo za ubingwa wa ligi hiyo.
Kwa sasa Simba inafundishwa na Mganda Jackson Mayanja aliyechukua nafasi ya Muingereza Dylan Kerr aliyetimuliwa licha ya timu hiyo kuwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo.
Mayanja alisema pamoja na ugumu wa mchezo huo, watajitahidi kuibuka na ushindi ili kuendelea kuzifukuza Yanga na Azam FC zilizoko kileleni. Coastal Union na African Sports ziko katika nafasi ya 14 na 15 baada ya kucheza mechi 15 na kuambulia pointi tisa na 10 badala ya kuwa na pointi 45 kutoka katika mechi hizo 15 za duru la kwanza.
Mechi zingine leo ni JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Majina ya Songea, huku Mtibwa Sugar wakiikaribisha Stand United, wakati Mwadui FC itaikaribisha Toto African wakati Kagera Sugar watacheza na Mbeya City na Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Ndanda FC.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa Mgambo kuikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. Kwa upande wa ufungaji mabao, Amis Tambwe ndiye anayeongoza hadi duru la kwanza linapomalizika baada ya kupachika mabao 13 huku Hamisi Kiiza wa Simba akifuatia kwa mabao 10.

Mahakama ya mafisadi yaiva

SERIKALI imewahakikishia Watanzania kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya mafisadi na wezi, umefikia hatua nzuri. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema hayo juzi bungeni mjini hapa, wakati akichangia Hotuba ya Rais ya Ufunguzi wa Bunge.
Akizungumzia mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo maalumu, Mwakyembe alisema unakwenda vizuri na utakapokamilika Watanzania watafahamishwa. “Kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, akitoa tamko lazima litekelezwe.
Kama tunakumbuka Rais, kwa nyakati tofauti kipindi cha kampeni, aliahidi kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi na Wezi,” alisema Mwakyembe. Akiizungumzia hotuba ya Rais, Mwakyembe alisema ikiachwa hotuba ya Mwalimu Nyerere, ya Magufuli pia ni bora na iligusa mioyo ya Watanzania wenye nia njema na Taifa.
“Wakati rais anatoa hotuba yake iliyokuwa na aya 160, alipigiwa makofi na vigelegele mara 137, ni zaidi ya asilimia 86, ya Dk Martin Luther ambaye ni Mmarekani mweusi,” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo, imewaweka pabaya wapinzani waliokuwa wanapinga kila kitu.
Dk Mwakyembe alisema tatizo ni kwamba kwa hotuba hiyo, yeyote akijaribu kuipinga, wananchi watamuona wa hovyo. Aliendelea kusema; “Wamejaribu (upinzani) kutoka kwenye mjadala, kwa hoja tu ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania), ili wasiwepo kwenye mjadala, kwani wakiwepo lazima wataisifia tu.”
January na Tanzania Mpya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), January Makamba alisema safari ya kutengeneza Tanzania Mpya, haitakuwa nyepesi na ni lazima wajaribiwe, watiwe shaka na kukatishwa tamaa kuhusu mwelekeo wao.
Akijibu hoja za wabunge zilizotolewa wakati wa kujadili hotuba hiyo ya Rais Magufuli ya ufunguzi wa Bunge, aliyoitoa Novemba mwaka jana, January alisema;“ni kama kutengeneza keki ya mayai, lazima upasue mayai”.
Aliendelea kusema, “watu wasipate mashaka wala wasiwasi kwamba nchi inaelekea katika mwelekeo usiofaa. Tulifika mahala tukahitaji Rais wa namna hii, tumempata na tumuunge mkono.”
Kauli ya Waziri inalenga kujibu kauli za baadhi ya watu, ikiwemo wabunge wa vyama vya upinzani, ambao hivi karibuni walikosoa kazi ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na Rais Magufuli pamoja na waziri, wakidai kwamba haizingatii taratibu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene alisema kazi ya Rais Magufuli ya kuisuka Serikali haijakamilika, kwani anaendelea kwa wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi hadi kwa wakuu wa idara, watakaochujwa kuhakikisha wanaendana ya kaulimbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’.
Alisema Tanzania mpya ya Magufuli inayokuja ni ya watu wanaofanya kazi. Tunataka tuwahakikishie kwamba Rais anaendelea kuisuka serikali na mtambue kwamba serikali bado haijakamilika, bado tunahitaji wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya lakini tunakwenda vizuri zaidi tunataka kusuka wakurugenzi.
“Tunakwenda mbali kusuka mpaka wakuu wa idara, tunataka tuwachuje vizuri kabisa na siyo kuokotana okotana. Tunataka Tanzania mpya tukianzia juu tukisema hapa kazi tu basi ni hapa kazi,” alisema.
Hotuba ya Rais Bungeni Akizungumzia Mapambano Dhidi ya Rushwa na Ufisadi, alipofungua rasmi Bunge mjini Dodoma, Novemba 20, mwaka jana, 2015, Rais Magufuli alisema, “Jambo moja nililolisemea kwa nguvu kubwa wakati wa kampeni ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Sikufanya hivyo kwa sababu nilitaka tu kuwarubuni wananchi ili wanipe kura zao na kunifanya kuwa Rais wao. Nililiongea jambo hili kwa dhati kabisa, na nilichokisema na kuwaahidi wananchi ndicho hasa nilichokikusudia. Wananchi wanachukia sana rushwa na ufisadi, na wamechoshwa na vitendo hivyo.
Mimi pia ninachukia rushwa na ufisadi. Sifurahishwi kabisa na vitendo vya rushwa na ufisadi vinavyoendelea hapa nchini. Vitendo vya rushwa na ufisadi vinawanyima haki wananchi na kuitia hasara serikali kwa mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya watu wetu.”
Magufuli alisema “Mimi nimewaahidi wananchi, na nataka nirejee ahadi yangu kwao mbele ya Bunge lako tukufu, kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi na bila haya yoyote. Dawa ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine.
Hivyo ninaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote mniombee na muniunge mkono wakati natumbua majipu haya.” Alieleza kuwa anafahamu ugumu wa vita aliyoamua kuipigana na anafahamu ugumu na changamoto zake kwa sababu wanaojihusisha na rushwa, sio watu wadogo wadogo.
Alisema Vitendo vya rushwa na ufisadi vyenye madhara makubwa kwa nchi na ustawi wa nchi yetu, hutendwa na watu wenye dhamana kubwa za uongozi na utumishi, ambazo wamezipata kutokana na ridhaa ya watu.
“Katika kushughulikia tatizo hili, nimeahidi kuunda Mahakama ya Rushwa na Ufisadi. Ni matumaini yangu vyombo husika katika jambo hili havitanikwamisha,” alisema Magufuli.

Hoja ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa yaondolewa bungeni

WAZIRI wa Fedha, Dk Philip Mpango ameondoa hoja ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano 2016/17 mpaka 2020/21 aliyoiwasilisha bungeni jana.
Hatua hiyo ilitokana na mwongozo uliotolewa kwa nyakati tofauti na wabunge; Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT Wazalendo) na wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).
Wabunge hao walisema Waziri amewasilisha hoja kinyume na kanuni za kudumu za Bunge, zinazosema katika mkutano wa bunge wa kila Oktoba na Novemba, Serikali inatakiwa kuwasilisha mpango wa maendeleo wa taifa wa kila mwaka.
“Kutokana na maelezo uliotoa (Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge) na kwa kutumia kanuni ya hamsini na nane, tano ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2016, naomba ruhusu kuondoa hoja niliyoiwasilisha leo (jana) asubuhi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano 2016/17 mpaka 2020/21,” alisema Dk Mpango.
Hoja hiyo iliondolewa baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Chenge kutoa mwongozo na kisha kuahirisha Bunge hadi kesho kutwa. Awali katika maelezo yao bungeni na nje ya Bunge, wakati wakizungumza na waandishi wa habari, Zitto na Lissu walisema uwasilishwaji wa hoja ya Waziri Mpango, umekiuka Katiba. Hata hivyo akitoa mwongozo, Chenge alisema suala hilo halikukiuka katiba.
“Nimelitafakari sana jambo hili, na baada ya kutafakari hakuna ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.” Alisema kilicholetwa na serikali ni mchakato wa kushirikisha wawakilishi wa Tanzania ili watoe maoni, ushauri na mapendekezo yao kuhusu na mpango unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika mwaka wa fedha 2020/16/17.
Alisema kitu ambacho wabunge lazima wakubali, ni kwamba kulingana na Kanuni ya 94 (1), Bunge linapofanya kazi hiyo huwa haliketi kama Bunge, bali linaketi kama kamati ya mipango. “Hiyo ni dosari ambayo tumeiona,” alisema na kukiri kwamba hapa ilikuwa ni mpango wa muda mfupi.
Hata hivyo alisema Ibara ya 63 haisemi ni lini huo mpango uletwe. Alikiri kuwa mpango mfupi unatokana na wa mwaka mitano, ambao hitimisho lake ni pale waziri atakaposoma mpango wa serikali kwa mwaka unaofuata wa fedha na jioni yake, Waziri anaposoma bajeti ya serikali.
Akihimiza kuwa Kanuni ya 94 (1) lazima izingatiwe, Chenge alisema, “Bunge halikuweza kukutana Oktoba na Novemba kama kanuni hiyo inavyotaka kwa sababu kulikuwa na shughuli kubwa ya uchaguzi.
Alisema Serikali na Bunge hawakuwa na njia nyingine, jambo ambalo ilikuwa lazima mchakato ufanyike sasa ili Machi 11, serikali iwasilishe mbele ya wabunge kama ilivyofanyika mwaka jana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
“Waziri mwenye dhamana anawasilisha mipango na ukomo wa bajeti. Wakishawasilisha, katibu wa bunge ndiye anapeleka kwa spika ili aelekeze ipelekwe kwenye kamati ya bajeti hadi watakapokuja kutoa taarifa,” alisema.
Kwa mujibu wa kanuni, siku ya kusoma bajeti ya serikali, waziri anawasilisha hoja yake ya mpango; utekelezaji wa hali ya mwaka jana na mwaka unaofuata. Hivyo kunakuwa na hoja mbili ambazo hujadiliwa kwa pamoja; hoja ya mpango na ya bajeti ya serikali.
“Haya ndiyo yanapaswa yafanyike,” alisema na kusihi wabunge kuelewa kanuni. Baada ya maelezo hayo, Chenge alimuita Waziri mtoa hoja; Waziri wa Fedha, aombe idhini ya Bunge ya kuondoa hoja. Kabla ya kutoa hoja hiyo, wabunge walihojiwa, na wote waliridhia.

Magufuli awateua Chagonja, Mtweve makatibu tawala

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi, ili kujaza nafasi za makatibu tawala wa mikoa hiyo. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema Dar es Salaam jana kuwa Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania. Balozi Sefue alisema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa Polisi, Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania. Aidha, Balozi Ombeni Sefue alisema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hao wa Polisi, kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.
Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Kuwait, wataapishwa jijini Dar es Salaam leo saa nne asubuhi.

Jumatatu, 25 Januari 2016

MAPENZI SHIDA PART 2

KWA HISANI YA OMBENI LONGO&HELMAN MHANGA

Baada ya JENIFER na wenzake kukamatwa na mwalimu na kupewa adhabu hiyo ya kwenda na wazazi wao shuleni siku ya Ijumaa tatu na kupelekea kupoteza mudi ya kuendelea kufurah usiku huo ikawabidi waondoke kabisa sehemu hiyo ya CLUB usiku huo huo na kwenda kulala kwenye chumba cha rafiki yao CHRISTINA waliekuwa nae katika kundi lao usiku huo, ilipofika kesho yake siku ya ijumaa pili asubuhi kila mtu alirejea nyumbani kwao huku wakiwa na sura za hudhuni na mawazo kibao kichwani wakijiuliza itakuaje kesho yake ambayo ni siku ya Ijumaa tatu wanatakiwa waende shule na wazazi wao?!. Jenifer alipofika kwao moja kwa moja alielekea chumbani kwake na kujilaza kitandani huku akiwa na mawazo kibao hata chakula hakuweza kula siku hiyo muda wote alikua kajifungia chumbani analia. Ghafla akasikia mlango wa chumbani kwake unafunguliwa aliposhtuka akamuona mama yake Mrs. Brown. Mrs. Brown alimsogelea binti yake Jenifer kuanza kuzungumza nae kama ifuatavyo:-
MRS. BROWN: "Jenifer binti yangu mbona unaonekana leo hauko sawa, nini tatizo mwanangu?! Na mbona unalia? 
JENIFER: "Hapana mama, wala usijali hamna kitu chochote naomba uwe na amani mama yangu, niko sawa tu!" 
MRS. BROWN: "Jenifer mwanangu lazima kutakuwa kuna kitu ila unaficha. Mwanangu nakuomba unieleze usinifiche niambie tu mwanangu wala usiogope" 
JENIFER: "Mama wala usijali hakuna kitu chochote kile" 
MRS. BROWN: "Sidhani binti yangu kama kweli hakuna tatizo sasa mbona unalia, Au umepata ujauzito?! 
JENIFER: "Mama bora ningekua nina ujauzito ila kwa hiki kilichonipata mama yangu najuta tena najuta hata sijui kwanini mlinipeleka shule mama yangu" 
MRS. BROWN: "Mwanangu mbona unasema hivyo kwani kuna tatizo limetokea shule?! 
JENIFER: "Ndio mama, kuna mwalimu shuleni alinitongoza nikamkatalia sasa kila siku huwa ananichapa fimbo bila makosa na ananitesa sana shule na kaniahidi kuwa atanitafutia kosa lolote la uongo ili nifukuzwe shule anikomoe na juzi siku ya Ijumaa kuna wanafunzi kawakamata usiku CLUB akawaambia kuwa atawafukuza shule sasa kaniambia namimi ataniingiza katika hilo kosa la hao wanafunzi kesho shuleni ili nifukuzwe namimi" 
MRS. BROWN: "Haiwezekani mwanangu wewe nyamaza acha kulia tumsubiri baba yako aje nimuelezee ikiwezekana kesho akupeleke shule akamkomeshe huyo mwalimu, wala usiwaze sana mwanangu Jenifer looooo, huyo mwalimu hana hata aibu" 
Baada ya Jenifer kutumia uongo wa kumdanganya mama yake Mrs. Brown kwa dhumuni la kujitetea kutokana na kosa alilolifanya usiku wa jana yake walipokutwa na mwalimu wao wa shule CLUB ikamlazimu kumpa kesi ya uongo yule mwalimu kwa wazazi wake ili wasimuone yeye anamakosa. Mama yake na Jenifer Mrs. Brown alihamaki na kuingiwa na hasira akawa anamsubiria mume wake arudi ili amuelezee kilichotokea. Ghafla baba yake na Jenifer Mr. Brown akaingia nyumbani kwake na kumkuta mke wake Mrs. Brown akiwa na binti yao Jenifer, Jenifer alipomuona baba yake Mr. Brown akaanza kuangua kilio huku akisema "BABA NAJUTA MIMI MWANAOO, NAJUTA BABA HIVI KWANINI ULINIPELEKA NIKASOME ILE SHULE BABA YANGUUUUUU" Jenifer alikua analia huku akitoa sauti kubwa ya kumlalamikia baba yake. Mr. Brown alipigwa na butwaa hakujua nini kinachoendelea ikabidi akae chini na kumuuliza mke wake "MKE WANGU NINI KIMEMPATA BINTI YETU JENIFER?" Mrs. Brown akamjibu mume wake "MUME WANGU NENDA KWANZA KAKOGE KISHA ULE HALAFU NDIO NIKUELEZEE KILICHOTOKEA" Mr. Brown nae akamjibu "HAPANA MKE WANGU NIELEZEE KWANZA NIJUE TATIZO NINI?". Mrs. Brown ikabidi aanze kumuhadithia kama alivyohadithiwa na binti yao Jenifer kuwa kuna mwalimu wa shule alimtongoza binti yao akamkataa sasa huyo mwalimu anamtesa sana Jenifer shuleni na kamuahidi atamfanyia njama yoyote ili binti yao afukuzwe shuleni. Pale pale Mr. Brown nayeye akapandwa na hasira akamnyamazisha binti yake Jenifer na kumwambia "JENIFER BINTI YANGU NYAMAZA, KESHO IJUMAA TATU ASUBUHI TUTAKWENDA WOTE MPAKA SHULENI KWENU UKANIONESHE HUYO MWALIMU. ATANITAMBUA" baada ya hapo wakatawanyika Jenifer akaingia chumbani akaanza kushangilia peke yake kimya kimya akiwa na imani kuwa kishamaliza kesi aliyokuwa nayo na akawa na furaha tele akaendelea kufanya mambo yake kama kawaida.

VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO TAR 25JANUARY 2016

MAPENZI SHIDA PART ONE

 Hadithi inayomuhusu binti wa kitanzania alietunukiwa uzuri wa asili na mvuto wa kipekee aliojaaliwa na mungu ama hakika uzuri aliokuwa nao ulikuwa ni kishawishi tosha kwa mwanaume yoyote aliemtazama binti huyu na kutamani kuwa nae kutokana na mvuto aliokuwa nao binti huyu anaitwa Jenifer na amezaliwa katika familia duni ya Mr. Brown na Mrs. Brown yenye watoto watatu (3). Ambao ni Peter, Joseph na Jenifer na katika watoto hawa watatu mwanamke alikua ni Jenifer peke yake na ndie alikua mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia hii yenye watoto watatu ambapo Peter na Joseph walikua ni wadogo zake na Jenifer na walikuwa bado ni wadogo sana. Na wazazi wa Jenifer Mr. Brown na Mrs. Brown walitokea kumpenda sana binti yao Jenifer kwani ndio mtoto pekee wa kike hivyo walionesha upendo mwingi kwa binti yao kwa kumtimizia mahitaj yote muhimu na kumpa kila alichokitaka binti yao ili wamridhishe na kuhakikisha wanampa malezi bora na kujenga upendo imara kwa binti yao. Kutokana na hali ya ngumu ya maisha iliyokuwepo katika familia hiyo ya Mr. Brown na Mrs. Brown, wazazi hawa walikaa na kujadili njia sahihi ya kuweza kukabiliana na umasikini walio nao na kuweza kujikwamua kimaisha wakapata wazo la kumpeleka shule binti yao Jenifer ili hapo baadae aje kuwasaidia wazazi wake kupitia elimu atakayoipata shule hivyo wazazi wakakubaliana na kuanza mipango ya kumuandikisha shule binti yao ili aanze kusoma, wazazi wa Jenifer walijitahidi kutafuta pesa kwa hali na mali ikapelekea wazazi wa Jenifer kujiunga na kampuni zinazotoa mikopo ya fedha lengo kupata pesa waweze kumtimizia mahitaji binti yao aweze kuanza shule. Mungu alileta kheri kwa wazazi hao na kufanikisha kuipata pesa ya kumpatia binti yao kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya shule na binti yao akafanikiwa kuanza elimu ya msingi akasoma darasa la kwanza mpaka darasa la saba lakini alipo maliza darasa la saba matokeo yake hayakua mazuri hivyo hakuweza kuchaguliwa katika shule za serekali kwa ajili ya kuendelea na elimu ya sekondari lakini wazazi wa Jenifer hawakukata tamaa na waliendelea kuwa na moyo wa kumsaidia binti yao Jenifer kwa vyovyote vile mpaka waone mwisho wake kwani malengo yao binti yao asome mpaka daraja la juu afike mpaka chuo kikuu, baada ya Jenifer kumaliza elimu ya msingi na hakufanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yake ikabidi wazazi wajipange upya kutafuta ada ya kumlipia binti yao ili aweze kujiunga na elimu ya sekondari kwa dhumuni la kuhakikisha binti yao Jenifer anaendelea na elimu. Mungu hakuitupa familia hii ya Mr na Mrs. Brown aliwajaalia wakafanikiwa kuipata pesa ya kumlipia ada binti yao na wakamuandikisha katika shule ya kulipia ya sekondari iliyofahamika kwa jina la "GARDEN SECONDARY SCHOOL" Jenifer alijiunga na shule hii na kuanza elimu yake ya sekondari lakini kama ilivyo kwa vijana wengi wa kisasa kutofahamu umuhimu wa elimu na kushindwa kujua nini wanapaswa kukifanya pindi wanapo kuwa shule ndivyo ilivyokuwa kwa Jenifer. Jenifer hakujua umuhimu wa elimu na hakuona juhudi za wazazi wake kwake za kutafuta pesa kwa ajili ya kumlipia ada ili aje kuwasaidia baadae na kuwasaidia wadogo zake Peter na Joseph. Kipindi Jenifer alipokua shuleni hapo akiendelea na elimu ya sekondari tabia yake ilibadilika akawa anautumia muda wake mwingi wa shule kujichanganya na marafiki ambao hawakuwa na msaada mzuri kwake na wakati mwingine alikua akiaga kwao anakwenda shule lakini alikua hafiki shule alikua anakwenda kwa marafiki anashinda na kurudi nyumbani wazazi wake hawakujua kinachoendelea kwa binti yao. Wakati mwingine Jenifer alikuwa ni mtu wa kupenda sana kwenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe wakati alikua anatoka nyumbani kwao usiku akiwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kwa marafiki zake anaosoma nao wanakwenda kukesha wakisoma na kujadiliana yale waliyofundishwa shuleni, wazazi wa Jenifer hawakuwa na kipingamizi kwa binti yao walikua ridhwaa kukubaliana na kila anachohitaji binti yao ili mradi kumridhisha na kumfanya awe huru ili mwisho wa siku aweze kutimiza ndoto za wazazi wake hivyo wazazi walikua wakimpa ruhusa binti yao atoke usiku wakidhani anaenda kusoma na wenzake kumbe Jenifer alikua anatumia muda huo kutoka na kwenda CLUB (kumbi za starehe) na marafiki zake wanaenda kujirusha na alikua anarudi nyumbani kwao kesho yake asubuhi, na ilikua kila ikifika siku ya Ijumaa mosi ndio anatoka usiku na wenzake, siku moja kama kawaida yake Jenifer na wenzake wametoka na kwenda kwenye kumbi za starehe huku nyumbani wazazi wanajua watoto wao wameenda katika masomo yao kama ilivyozoeleka, kipindi wapo CLUB kuna mwalimu wao wa shule alikuwepo katika ukumbi huo wa starehe na akakutana na kundi hili la wakina dada kama wanne akiwemo na Jenifer wakiwa wamevaa mavazi mafupi ya ajabu kama machangudoa wanaojiuza, yule mwalimu wao alichokifanya akawaita kisha akawaambia "NAOMBA SIKU YA IJUMAA TATU MKIFIKA SHULE CHA KWANZA NAOMBA NIWAKUTE OFISINI KWANGU KAMA MLIVYO WANNE TENA MJE MKIWA MMEVAA HIZI NGUO MLIZO ZIVAA NA KILA MMOJA WENU AJE NA MZAZI WAKE" kisha mwalimu akawaambia wawe huru waendelee na mambo yao ila ikifika siku ya Ijumaa tatu siku ya shule wafanye kama alivyo agiza mwalimu huyo pale pale Jenifer na wenzake wakakosa amani na mudi ya kuendelea kufurahi usiku ule ikatoweka na kila mmoja wao akawa anawaza itakuaje hiyo siku ya Ijumaa tatu na wataanzia wapi kuwaeleza wazazi wao juu ya kosa hili walilofanya mpaka wamekutana na mwalimu kawaomba waende shule na wazazi wao.....?!

Jumapili, 10 Januari 2016

ngoja ngoja utakuta mwana si wako

1st year

nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why

2nd year

Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

3rd year

Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda.
katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Graduation Day

siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it.
kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Miaka michache baadae

Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it.
but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.

Kwenye Mazishi

Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'

Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi
I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me!

Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!!

Vunja ukimya

Karibu elimumsingi bila malipo


KAMA Mzazi inapenda kuanza mwaka huu mpya wa 2016 kwa kuwapongeza wote waliobahatika kwa mapenzi ya aliyetuumba kuwa hai na salama na kuendelea kuomba Mungu awalinde kwa mwaka huu tangu mwanzo hadi mwisho wake.
Tunawajibika kushukuru kwa sababu kuna wenzetu hawakubahatika kuuona mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wetu. Lakini kubwa kwa Januari hii ya 2016 ni zawadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa wazazi na walezi kwa kuanzisha elimumsingi bila malipo kwa vitendo.
Elimumsingi inajumuisha elimu ya awali,ya msingi na sekondari, kuwa bure kwa gharama za serikali kwa shule za ngazi hiyo zinazomilikiwa na serikali ispokuwa shule 11 tu nchi nzima. Hongera sana serikali ya Rais Magufuli kwa kuishi kwa vitendo.
Kwa mujibu wa waraka wa serikali uliotolewa katikati ya Desemba mwaka jana, uliainisha wazi majukumu ya serikali katika utekelezaji wa elimumsingi bila malipo lakini pia ulioanisha majukumu ya wazazi katika utekelezaji wa jambo hili ili watoto waweze kusoma bila kupata changamoto zisizo za lazima.
Kama Mzazi nataka kuwakumbusha majukumu ya wazazi na walezi katika utekelezaji wa jambo hili kwani yale ya serikali, yenyewe inayajua vilivyo na tayari imeshaanza kutekeleza kwa kutenga fedha za kugharimia elimu hiyo.
Wazazi na walezi kwa mujibu wa waraka wa serikali wanatakiwa kununua sare za shule na vifaa vya michezo,vifaa vya kujifunzia ikiwa ni pamoja na daftari na kalamu, vifaa vya usafi binafsi, chakula kwa wanafunzi wa kutwa na bweni na gharama za matibabu.
Gharama nyingine kwa wazazi na walezi ni kulipia nauli ya kwenda na kurudi shule kwa wanafunzi wa kutwa na wanafunzi wa bweni kwa wakati wa likizo, kununua magodoro, shuka na vifaa vya usafi.
Ili kuhakikisha kwamba hayo yanafanyika bila kuleta manung’uniko kwa kutumbukiza gharama zisizokuwemo katika orodha hiyo, wazazi na walezi wanatakiwa kukemea na kutoa taarifa kwa vyombo husika juu ya mienendo inayokwenda kinyume na utaratibu wa elimumsingi bila malipo.
Kwa uhalisia wake kila mzazi na mlezi anatakiwa kuwa macho kwa kuwa msimamizi wa utekelezaji wa sera hiyo ya serikali ya elimumsingi bila malipo huku watoto wakibakiwa na jukumu la kusoma kwa bidii na uwezo waliojaliwa kwa ajili ya kujipatia ufunguo wa maisha yaani elimu. Visingizio na figisufigisu zisipewe nafasi katika hili ili tuweze kunufaika vilivyo.
Visingizio vya watoto kutokwenda shule kwa sababu ya wazazi au walezi kushindwa kumlipia ada mwanafunzi katika ngazi hizo tatu visipewe nafasi kama ilivyokuwa kabla ya utaratibu huu mpya. Kila mmoja wetu, hususan ni wazazi na walezi wajiandae kwa gharama zilizoorodheshwa ili watoto wetu wote waingie madarasani kwa kazi moja ya kujifunza. Hapa Kazi Tu sasa!

Jumamosi, 9 Januari 2016

Prof. Ndalichako ameipa NECTA siku 7 itoe maelezo kwanini mfumo wa kupanga matokeo kwa GPA ni bora kuliko wa Divisheni uliokuwa unatumika tokea awali.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limpe sababu za kubadili mfumo wa utunuku viwango vya ufaulu wa awali( Division) na kwenda wa wastani wa pointi (GPA) unaotumika sasa Kidato cha Nne na Sita.

Aidha, ametaka litoe maelezo ya kitaalamu juu ya sababu za kuanzisha mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea na kwamba zisipomridhisha, mwaka huu wasifanyishwe mtihani huo.

Mfumo wa GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka 2014 ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana.Vile vile mitihani miwili kwa watahiniwa wa kujitegemea, ilianza mwaka 2014 na 2015.

Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa baraza hilo kwa miaka tisa, alitoa maagizo hayo jana ambako pamoja na masuala mengine, alishuhudia namna alivyojaribiwa na kuletewa vishawishi jambo ambalo alisema, alilishinda kwa kusimamia taaluma.

Maagizo hayo aliyatoa alipotembelea na kuzungumza na viongozi, wafanyakazi wa NECTA ambako hakuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde.

Alisema tangu alipoteuliwa kuwa Waziri, amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa elimu na wananchi juu ya mfumo wa sasa wa upangaji matokeo wa GPA ambao umekuwa haueleweki na kwamba hawakushirikishwa katika mabadiliko hayo.

“ Nataka nijue sababu za kitaalamu za kubadilisha mfumo wa upangaji wa matokeo kutoka kwenye ule wa Division (madaraja) kwenda kwenye ule wa GPA na kama huo mfumo una tija kwa elimu yetu,” alisema.

Awali , Dk Msonde alisema mfumo huo ulipitishwa baada ya vikao kati yake, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Vyuo vya Ufundi (Nacte) na Wizara.

Alisema baraza lilitakiwa kuendesha mfumo huo ili kwenda na mifumo mingine ya elimu ya juu katika kurahisisha udahili wa wanafunzi kwenda sanjari na mfumo wa serikali mtandao na ajira.

Watahiniwa kujitegemea
Kuhusu uanzishwaji wa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea, Ndalichako alisema, “Nataka sababu za watahiniwa wa kujitegemea kupewa mtihani wa pili ambao unachukuliwa kama alama upimaji endelevu kwa mwanafunzi.

“ Kama baraza ambalo ndio wataalamu, mnasema mmeamua kutoa mtihani wa pili kutokana na kupokea malalamiko ya kufeli na mtihani mgumu, basi hatuwezi kuendelea nao, nataka nipate sababu za kitaalamu na kama sababu haziridhisha basi mwaka huu wasifanyishwe mtihani wa pili,” alisema.

Alisema kwa kawaida, mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea hauwezi kuwa mbadala wa alama endelevu kwa wanafunzi. Alisema unaongeza mzigo kwa watahiniwa na gharama za kulipa wasimamizi na wasahihishaji wa mitihani hiyo.

Ashuhudia alivyojaribiwa
Ndalichako aliwataka viongozi wa baraza hilo kutokukurupuka katika kutoa uamuzi na kufanya mabadiliko yasiyo na tija kwa taifa. Badala yake, alisisitiza watumie utaalamu wao kushauri na kukataa maagizo yasiyo na tija kusaidia katika kuboresha elimu.

Katika hatua nyingine, Ndalichako aliwataka watendaji wa Baraza hilo kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu na kuepuka vishawishi. “ Baraza la Mitihani ni sehemu ngumu sana, hasa kutokana na kuhudumia watu na hasa katika suala zima la mitihani.

"Na ni eneo ambalo lina vishwishi vingi, hata mimi nilijaribiwa kuletewa vishawishi lakini nilisimama misimamo ya taaluma,” alisema.

Ndalichako pamoja na kuwapongeza Baraza kwa kutoa vyeti mbadala, ametaka kuwa makini katika suala hilo kuzuia udanganyifu.

Alisisitiza watoe tathmini ya kina katika matokeo ya wanafunzi ambayo yatasaidia wizara kufanya uboreshaji. “Nilipokuwa hapa, kuna wakati nilikuwa nakosa usingizi linapokuja suala la kutangaza matokeo, unakuta matokeo ya wanafunzi 30 yote ni mbaya, sasa hapa si kuwa wanafunzi wote walikuwa hawafundishiki ila kuna tatizo la ziada, na hilo ndio tunatakiwa kushughulikia,” alisema.

Alisema, “ Nilikuwa naumia sana na ubora wa elimu iliyokuwa ikitolewa kwa baadhi ya shule, sasa nimepewa kazi ya kuhakikisha elimu inakuwa bora, tunaondoa watu wa kuchora mazombi na ule wakati wa shule kugeuka vituo vya kulelea watoto badala ya kutoa elimu umefika mwisho.”

Yanga SC yamkuna Pluijm

KOCHA wa timu wa Yanga, Hans Van Pluijm amesema kuwa ameridhishwa na kiwango kinachoendelea kuoneshwa na wachezaji wake katika michuano ya Kombe la Mapinduzi mjini hapa.
Yanga imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza michezo ya makundi wakiwa na pointi saba na kushika nafasi ya kwanza katika msimamo wa kundi A huku Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi nne.
Akizungumza baada ya kumaliza mchezo baina yake na Mtibwa, Pluijm alisema kuwa wachezaji wake wanacheza kwa jinsi alivyowaelekeza. “Naridhika na kiwango chao hasa kwa vile wanafuata maelekezo yangu na wanacheza vile ninavyotaka wacheze,”alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi ni mazuri kutokana na kuwa na ushindani ambao unazidi kuongeza uimara wa timu yake. Katika mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 2-1 na mabao yake yalifungwa na Yussuf Abubakar dakika ya 42 na Mwalimi Busungu dakika ya 82, wakati lile la Mtibwa lilifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 10. I

Magufuli ampa 5 Samatta

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amemtumia salamu za pongezi mshambuliaji wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Magufuli alituma salam hizo jana kupitia Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari, Dk Magufuli alimtumia salamu za pongezi Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye afikishe salamu zake za pongezi kwa Samatta.
“Rais Magufuli amemtaka Waziri Nnauye amfikishie salamu zake za pongezi kwa mchezaji huyo, ambaye pia anaichezea TP Mazembe,” imesema taarifa hiyo ikiongeza kuwa tuzo hiyo imejenga heshima kwa Samatta na Tanzania.
Katika taarifa hiyo, Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi kuuendeleza mchezo ili upige hatua zaidi kimaendeleo. Samatta alitwaa tuzo ya mchezaji bora juzi usiku iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) katika sherehe zilizofanyika Abuja, Nigeria.
Mchezaji huyo alikuwa akipambana na wachezaji wengine wawili ambao ni Robert Kidiaba Muteba (wa TP Mazembe na Congo) na Baghdad Bounedjah (Algeria & Etoile du Sahel).
Samatta alipata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa Kidiaba wa DRC aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Bounedjah alipata pointi 63.
Mchezaji huyo wa Tanzania ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa ya Afrika. Mafanikio hayo yamekuja baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake manane.
Mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya kwanza na kumshinda Yaya Toure wa Man City na Ivory Coast aliyekuwa akisaka tuzo hiyo kwa mara ya tano.
Aubameyang wa Borussia Dortmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 26, amewaangusha Toure aliyekuwa anashikilia tuzo hiyo na Andre Ayew wa Ghana. Amekusanya pointi 143, saba zaidi ya Toure wakati Ayew ameshika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 112.
Wakati huo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametoa pia pongezi zake kwa mchezaji huyo. Naye, Kocha wa Yanga, Hans Pluijm amempongeza Samatta kwa tuzo hiyo akisema kuwa, itawatia moyo wachezaji wengine wa ndani wa Tanzania kubadilika katika mtizamo wa kucheza soka la kulipwa.
“Tuzo hiyo itawafanya wachezaji wengine wa Tanzania kucheza katika kiwango cha juu sio tu katika kujipandisha wao wenyewe, bali kuisaidia timu ya taifa hasa katika mashindano ya kimataifa,” alisema.

Bomoa bomoa iko pale pale

SERIKALI imesema ubomoaji na uondoaji wananchi waishio katika Bonde la Mto Msimbazi utaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi. Watakaohusika na uhamishwaji huo, sasa ni wale tu ambao makazi yao yapo ndani ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye kingo za mto.
Imesisitizwa, awamu hii ya ubomoaji, itajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu na watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga.
Maamuzi hayo yamefikiwa juzi baada ya mawaziri watatu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI); Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Mawaziri hao walifanya mkutano wa kutathmini uhamishaji wa wakazi wa mabondeni katika jiji la Dar es Salaam. Waliamua kuwa watumishi wa umma waliowamilikisha wakazi maeneo hayo, watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Taarifa ya maamuzi hayo ilitolewa jana na Ofisi ya Makamu wa Rais. Pia, taarifa hiyo ilisema mawaziri hao wameamua katika siku tatu zijazo, serikali itaanza kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.
Mawaziri hao walibainisha kuwa serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni, lakini pia itafuatilia kesi hizo ziishe haraka ili taratibu zinazofuata zifanyike.
“Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali imeanzisha dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hilo.
Walisema nyumba na majengo yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa sheria zinazotekelezwa katika ubomoaji huo hayatabomolewa, isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini.
Vile vile ilisema wanaoishi katika makazi hayo, watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa, kwani serikali haina dhamira ya kubomoa hoteli kubwa za siku nyingi zilizo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa hoteli hizo, watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.
Pia, serikali inaweka utaratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi, zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii. “Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi.
Lakini, pia haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini,” ilisisitiza taarifa hiyo. Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea miaka ya hivi karibuni. Tathmini ya ubomoaji huo iliyotolewa ripoti kwa mawaziri hao, ilieleza kuwa hadi sasa wananchi katika nyumba 774 wamehama na nyumba hizo kubomolewa.
Taarifa hiyo ilieleza pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi, hivyo hawakuhamishwa.
Nchi ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi, ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao, lakini kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
Taarifa hiyo ilisema sababu za kufanya usafishaji wa mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka, unalenga kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Eneo la Bonde la Mto Msimbazi, lilitangazwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979, hivyo usafishaji huo utapanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa na kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi.
Taarifa hiyo ilisema kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili, ndizo zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomolewa, baada ya hapo mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.
“Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe, baada ya hapo alama huwekwa kuonesha mpaka wa bonde,” ilisisitiza taarifa hiyo.
Pia, taarifa hiyo ilieleza kwamba imebainika sehemu kubwa ya wakazi wa mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wanakaa sehemu nyingine salama. Suala la Mchungaji Rwakatare Taarifa ya mawaziri hao pia ilieleza kuhusu suala la Mchungaji Getrude Rwakatare.
Ilisema mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) amefukuzwa kazi Januari 6 mwaka huu na taarifa zake zimekwishafikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokana na tuhuma za kufanya udanganyifu kwa niaba ya Baraza, kwa lengo la kumlinda Mchungaji huyo wa kiroho.
Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais imeshafungua upya kesi mahakamani kuanzia Desemba 29 mwaka jana, kuomba “makubaliano” kati ya mwanasheria huyo wa NEMC na Mchungaji Rwakatare, yawekwe pembeni kwa sababu yalipatikana kwa njia ya udanganyifu.
Taarifa hiyo ilisema Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake mahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume na sheria tatu muhimu.
Ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza, jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za serikali za mitaa, lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. NEMC ilipoingilia kati na kutaka kubomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani na wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, Mei 11 mwaka jana aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.
Ilielezwa kuwa makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu Mei 13 mwaka jana, kisha Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba mwaka jana, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza.
Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (DART) Taarifa hiyo ilisema mkutano wa mawaziri hao, ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira Kifungu 57 (2) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi au shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni.
Hivyo, waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo, zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira. “Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira, zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Mawaziri walitaka kufahamu hayo kutokana na hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni, lakini mradi wa DART umeachwa.

Wasiopeleka watoto shule kuburuzwa kortini Machi


SERIKALI imesema haitosita kuwafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani ifikapo Machi 30, mwaka huu, wazazi ama walezi wote watakaoshindwa kupeleka watoto wao shuleni ili kupata elimu ya msingi na sekondari.
Aidha, imepiga marufuku kwa jamii kutumia jina la ‘watoto wa majumbani’, badala yake waitwe wasaidizi hao ‘wasichana wa kazi’ au ‘vijana wa kazi’. Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Dar es Salaam jana.
Alisema hayo ili kuhamasisha wazazi na walezi juu ya watoto kujiunga na shule za msingi na sekondari kwa mwaka huu 2016. Kuhusu kuwafungulia wazazi mashtaka, alisema serikali inaamini kuwa ikiwa inataka kujenga taifa lililoelimika ni lazima kuwekeza kwenye elimu, hivyo ni wajibu wa kila anayehusika kuhakikisha anatimiza wajibu wake.
“Elimu ndio njia bora ya kuwajengea watoto wetu msingi imara wa maisha yao…serikali haitosita kuchukua hatua za kisheria kwa wazazi au walezi ambao watazembea, kumficha, kumtorosha au kuzuia mtoto kuanza masomo ya shule za msingi na sekondari,” alisema Ummy.
Alisema serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itawafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote watakaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule, kwani hata Sheria ya Mtoto Namba 2 ya mwaka 2009 Kifungu cha 8, inaelekeza kuwa ni wajibu wa mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu.
Waziri Ummy alisema Kifungu cha 14 kinatamka kuwa ni kosa la jinai, kushindwa kutimiza wajibu huo na adhabu yake ni faini isiyozidi Sh milioni 5 na kifungo kisichozidi miezi 6; au vyote kwa pamoja.
Alisema pia wazazi na walezi, wahakikishe kuwa watoto wanaoendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari, wanahudhuria masomo yao kwa ufanisi, kwa kuwa serikali haitarajii kuendelea kuona utoro wa watoto shuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.
Kuhusu kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa watoto wanaoanza masomo, alisisitiza kuwa wazazi, walezi na jamii kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kuanza elimu ya msingi yaani darasa la kwanza na elimu ya awali, kujiunga na shule kwa muda uliopangwa na kuhudhuria masomo ipasavyo.
Kuhusu kuwepo kwa michango mbalimbali katika baadhi ya shule wakati huu wa maandalizi ya shule, alisema serikali imeshatoa mwongozo stahiki. Waziri huyo alisisitiza kwamba sio ada peke yake iliyofutwa, bali hata michango yote na tayari serikali imekwishatoa fedha za kugharimia elimu bure na zimekwishapelekwa katika shule zote nchini.
Kwa ujumla, walimu wakuu hawatakiwi kutoza mchango wa aina yoyote, kama vile ya ulinzi, maji, umeme, uzio, fagio, jembe, ndoo na mingineyo, kwani fedha za kugharimia elimu ya bure zitatumika pia kwenye masuala hayo yote

Ijumaa, 1 Januari 2016

Magufuli ateua makatibu wakuu 29, manaibu 21

Thursday, December 31, 2015


Rais John Magufuli 
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wa wizara mbalimbali.
Aidha, Dkt Magufuli pia amemteua Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kutengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Lusekelo Mwaseba.
Miongoni mwa Makatibu walioteuliwa ni pamoja na nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye amebaki Balozi Ombeni Sefue.
Baadhi ya Makatibu waku hao waliochaguliwa ni pamoja na Mhandisi Mussa Iyombewa ameteuliwa katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ofisi ya Makamu wa Rais anakuwa Mbaraka A. Wakili.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano waliochaguliwa ni Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu – Ujenzi), Dokta Leonard Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi) na Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano).
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni Dokta Yamungu Kayandabira, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ni Maimuna Tarishi.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wanakuwa ni Dokta Mpoki Ulisubisya atakayesimamia Afya na Sihaba Nkinga - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Wizara ya Nishati na Madini ni Profesa Justus W. Ntalikwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ni Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira.
Wizara ya Fedha na Mipango anabaki kuwa Dokta Silvacius Likwelile , Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ni Dkt Aziz Mlima. Huku Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiteuliwa Job D. Masima.

Maxime amlalamikia mwamuzi


BAADA ya Mtibwa Sugar kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Azam, Kocha Mecky Maxime amemlaumu mwamuzi wa mchezo huo akidai aliwabeba wapinzani wao.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi juzi, bao pekee la Azam lilifungwa na John Bocco.
Akizungumza baada ya mchezo huo Maxime alisema mwamuzi Ngole Mwangole ambaye alikuwa akichezesha mchezo huo alikuwa akitafuta namna ya kuipa ushindi Azam.
“Ukiangalia kwa mfano faulo iliyotolewa kwa Azam na Mwangole haikuwa ya haki, wanadai Bocco alitendewa madhambi na Salim Mbonde katika eneo la hatari, lakini ukiangalia halikuwa kosa,” alisema.
Alisema kikosi chake kilicheza vizuri mechi hiyo isipokuwa mchezo uliharibiwa na mwamuzi huyo na kuvuruga baada ya kupata kipigo hicho. Maxime alisema mara nyingi waamuzi wamekuwa wakiharibu mpira hata kama timu imeanza vizuri.
“Timu zote zilicheza vizuri inavyotakiwa lakini refa tu aliharibu mpira, alikuwa anatafuta kitu na ndio alichokifanya kwa sababu mchezaji wangu ndio alianza kushikwa,” alisema.
Alieleza kuwa waamuzi imekuwa tatizo la muda mrefu na wanachangia kuua soka nchini kutokana na kufanya makosa yanayojirudia bila kuchukuliwa hatua yoyote.
Alisema halalamiki kwa kuwa amefungwa kwani ni sehemu ya mchezo isipokuwa afungwe kihalali.

Yanga, Azam kamili kwa Mapinduzi

YANGA na Azam FC zinatarajia kuondoka leo kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza keshokutwa mpaka Januari 13 kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili jana Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe alisema timu yao inaondoka na wachezaji wote isipokuwa Nadir Haroub ambaye ni majeruhi. “Mchezaji ambaye hataungana na sisi ni Haroub peke yake ambaye ni majeruhi,” alisema.
Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa Kundi B pamoja na Azam FC, Mtibwa Sugar na Mafunzo, wakati Kundi A lina timu za Simba, ambao ni mabingwa watetezi, URA ya Uganda, JKU na Jamhuri ya Pemba.
Yanga watafungua dimba kwa kucheza na Mafunzo keshokutwa, mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC usiku. Mabingwa watetezi, Simba SC watateremka uwanjani kwa mara ya kwanza Januari 4, kumenyana na Jamhuri usiku, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya URA na JKU.
Nusu fainali zitachezwa Januari 10, wakati fainali itachezwa Januari 13 sambamba na kilele cha sherehe za Kombe la Mapinduzi 2016.

Wasomi wapongeza makatibu wakuu

  Imeandikwa na Waandishi Wetu
WAKATI makatibu wakuu wateule na manaibu wao wanaapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam, baadhi ya wasomi wamesema uteuzi wao ambao ameufanya Rais John Magufuli unalenga kuisaidia nchi iweze kuingia kwenye uchumi wa Viwanda.
Profesa Emrod Elisante wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) alisema kwamba uteuzi huo ni mzuri kwani umezingatia utaalamu zaidi. Alisema lazima wizara ziwe na wasimamizi madhubuti ambao wataisaidia nchi kuwa yenye viwanda.
“Nikiwaangalia watu kama Dk Chamriho (Leonard, Katibu mkuu Uchukuzi) Profesa Mkenda (Adolf, Katibu mkuu katibu Mkuu Biashara na Uwekezaji) hawa ni watu makini na ni watendaji wazuri naamini wataisaidia nchi,” alisema.
Alisema iwapo watapewa malengo na rais, wana uwezo wa kuyatekeleza hasa kuifanya Tanzania iwe sekta ya viwanda kama alivyoahidi Rais Magufuli wakati wa kampeni.
Profesa Elisante alisema licha ya nchi kuwa na changamoto mbalimbali kama za kifedha na rasilimaliwatu, lakini alisema uteuzi huo umejaa wataalamu ambao wengi wamepelekwa kwenye fani zao.
“Unajua hata waliopita ni wazuri, ila tatizo waliingia kwenye siasa, Rais Magufuli akiweza kuwadhibiti hawa wasiingie kwenye siasa na wakafanya kazi yao kwa weledi na kujua malengo ya wizara na nchi naamini tutachomoka,” alisema.
Naye Mwanaharakati za haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa alisifu uteuzi wa makatibu wakuu hao kwa maelezo kuwa umewapeleka watu katika fani walizosomea.
“Mfano Profesa Mchome (Sifuni ambaye ni Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria) yule ni mwanasheria aliyebobea naamini ataisaidia nchi kwa kutumia taaluma yake,” alisema Olengurumwa.
Alisema kitendo cha Rais Magufuli kujaza wataalamu kama maprofesa na madaktari katika Serikali yake kunaonesha kuwa anathamini wataalam hao na angependa kuona wanatumia taaluma yao kuisaidia nchi.
“Utakuta katika wizara kwa mfano ya Madini, kuanzia Waziri hadi makatibu wakuu ni profesa na daktari, wakikaa pamoja wanaweza kufanya vizuri lakini pia wanaweza kufanya vibaya,” alisema Olengurumwa.
Alisema dhamira ya rais ni nzuri, hata hivyo alikosoa wingi wa makatibu wakuu hao hasa uteuzi wa manaibu makatibu wakuu kuwa haukuwa na maana kwani kila kitengo na idara kina mkurugenzi ambaye kama katibu mkuu hayupo anaweza kufanya kazi zake.
“Alipunguza baraza la mawaziri tukafurahi, lakini amerudi nyuma kwa kuleta makatibu wakuu wengi tofauti na alivyotangaza kuwa makatibu wakuu pia wangepungua, kwa hiyo tuko kule kule,” alisema Olengurumwa.
Naye Katibu Mkuu mteule wa Afya katika wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya amesema ameupokea uteuzi wake kwa mshituko mkubwa kwa kuwa ni jambo ambalo hakuwahi kulifikilia.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake ya Ukurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dk Ulisubisya alisema uteuzi wake umekuja kwa ghafla huku akiwa na mipango aliyokuwa amejiwekea ya kuendeleza hospitali hiyo.
Alisema mawazo yake yote ilikuwa ni kujipanga kuhakikisha anatekeleza majukumu aliyokuwa ameachiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii majuma mawili yaliyopita, Dk Donan Mbando aliyefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo.
Dk Ulisubisya alisema agizo lingine lilikuwa kuhakikisha hospitali hiyo inaanzisha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuongezea taaluma kwa madaktari na kuboresha huduma za dharura na kupunguza foleni kwa wagonjwa, mambo ambayo tayari alianza kuyafanyia kazi na kuyawekea mikakati.
Wakati huo huo, leo Rais Magufuli anawaapisha makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali aliowateua juzi. Kazi ya kuwaapisha inafanywa leo Ikulu na kwa hatua hiyo, Rais atakuwa amekamilisha kazi ya kupata watendaji wa ngazi za juu katika wizara mbalimbali, ambazo ni moja ya vyombo vinavyotegemewa kuleta maendeleo ya watanzania ikiwa kila mmoja kwa nafasi yake, atatimiza wajibu wake. Imeandikwa na Shadrack Sagati, Dar na Joachim Nyambo, Mbeya.