Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa
dharura, jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa,
Freeman Mbowe, ambapo pamoja na masuala mengine, itapokea taarifa na
kujadili hali ya siasa nchini.
Katika
siku za hivi karibuni, taifa limekuwa likipitia katika majaribu
makubwa, ikiwa ni pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za
kuongoza nchi unaofanywa waziwazi na mamlaka za juu/viongozi waandamizi
wa nchi kupitia kauli na matendo mbalimbali kiasi cha kuwashtua
Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao ikiendeshwa katika misingi ya
uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.
Katika
kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24, mwaka huu, Kamati Kuu pia
itapokea taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu mipango
mbalimbali inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya
shughuli zake kwa ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha misingi
kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima, kupitia usimamizi wa kanda 10 za
chama.
Imetolewa Ijumaa, Julai 22, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni