ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 6 Julai 2016

#MAGAZETINl:Waziri Kairuki ateua Ma-DAS wapya nchini

OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumioshi wa Umma na Utawala Bora imejaza nafasi zilizokuwa wazi za Makatibu Tawala wa Wilaya (Ma-DAS) katika wilaya mbalimbali nchini.
Kujazwa kwa nafasi hizo kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya Ma-DAS kustaafu, kufariki pamoja na kupoteza sifa za kuendelea kuwa makatibu tawala wa wilaya hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alisema, baadhi ya wilaya zimeachwa wazi ambapo uteuzi wa Ma-DAS utafanyika baadaye kwa ajili ya kujaza nafasi hizo.
Kairuki alizitaja wilaya hizo na mikoa yake kwenye mabano kuwa ni Newala (Lindi), Makete (Njombe) pamoja na Kisarawe iliyopo mkoa wa Pwani.
“Makatibu ambao waliokuwepo wataendelea na kazi kama kawaida lakini kwa wale wapya walioteuliwa wafike ofisi za Utumishi wakiwa na CV (wasifu zao pamoja na nakala za vyeti vyao,” alisema Kairuki.
Ma-DAS walioteuliwa na Wilaya na Mikoa yao kwenye mabano ni David Mwakiposa (Arusha), Amos Siyantemi (Monduli), Adam Mzee (Arumeru), Abas Kayanda (Karatu), Lamuel Kileo (Ngorongoro) na Toba Nguvila (Longido, Arusha).
Kwa mkoa wa Dar es Salaam walioteuliwa ni Edward Mpogoro (Ilala), Omary Mhando (Kigamboni), Mtela Mwampamba (Ubungo), Hashimu Komba (Temeke) na Gift Msuya (Kinondoni). Dodoma walioteuliwa ni Kasilda Mgeni (Bahi), Athanasia Kabuyanja (Mpwapwa), Juliana Kilasara (Chamwino), Audiphace Mushi (Kongwa), Winnie Kijazi (Kondoa), Jasinta Mboneko (Dodoma) na Ally Chilukile (Chemba).
Geita walioteuliwa ni Thomas Dime (Geita), Paul Cheyo (Bukombe), Eliasi Makory (Chato), Reuben Mwelezi (Nyang’wale) na Christopher Bahali (Mbogwe). Iringa ni Allan Mwella (Mufindi), Joseph Chitika (Iringa) na Yusuph Msawanga (Kilolo).
Katavi ni Epaphras Tenganamba (Mlele), Mahija Nyembo (Mpanda) na Mwashitete Geogrey (Tanganyika). Kagera ni Gread Ndyamukama (Bukoba), Joel Mwakabibi (Biharamulo), Josephat Tibaijuka (Ngara), Mwakasyege Richard (Muleba), Godfrey Kasekenya (Misenyi), Weka Ng’olo (Karagwe) na Haji Godigodi (Kyerwa).
Kigoma ni Muguha Muguha (Kasulu), Kwame Daftari (Kigoma), Ayubu Sebabili (Kibondo), Zainab Mbunda (Kakonko), Upendo Marango (Uvinza) na Peter Masindi (Buhigwe).
Kilimanjaro ni Heri James (Hai), Abubakari Asenga (Rombo), Mabenga magonera (Same), Yusufu Kasuka (Mwanga), Leornad Maufi (Moshi) na Nicodemus John (Siha).
Lindi ni Thomas Safari (Lindi), Lameck Lusesa (Liwale), Athanas Hongoli (Kilwa), Husna Sekiboko (Nachingwea) na Twaha Mpembenwe (Ruangwa). Manyara ni Ndaki Mhuli (Kiteto), Zuwena Omary (Simanjiro), Mkumbo Barnabas (Hanang), Cade Mshamu (Babati) na Samuel Gunzar (Mbulu).
Mara ni (Justin Manko (Musoma), Masalu Kasasila (Bunda), John Mahinya (Tarime), Cosmas Qamara (Serengeti), Mirumbe Daudi (Rorya) na Credo Lugalila (Butiama). Mbeya ni Anold Mkwawa (Mbeya), Moses mashaka (Rungwe), Ezekia Kilemile (Mbarali), Sostenes Mayoka (Chunya) na Godfrey Kawacha (Kyela).
Morogoro ni Alfred Shayo (Morogoro), Michael Maganga (Mvomero), Stanslaus Nyanga (kilosa), Linno Mwageni (Kilombero), Abraham Mwaikwila (Ulanga/ Mahenge) na adam bibangamba (Gairo). Mtawara ni Teoford Ndomba (Mtwara), Benaya Kapinga (Masasi), Azizi Fakili (Tandahimba) na Michael Matomola (Nanyumbu).
Mwanza ni Kazeri Japhet (Misungwi), Solomon Ngiliule (Magu), Andrea Ng’hwani (Kwimba), Allan Muhina (Sengerema), Yonas Alfred (Nyamagana), Focus Majumbi (Ukerewe) na Tryphone Mkorokoti (Ilemela). Njombe ni Joseph Chota (Njombe), Stephen Ulaya (Ludewa) na Edward Manga (Wanging’ombe).
Pwani ni Erica Yegella (Bagamoyo), Sozi Ngate (Kibaha), Gilbert Sandagila (Mafia), Severine Lalika (Mkuranga) na Maria Katemana (Rufiji).
Rukwa ni Festo Chonya (Nkasi), Christina Nzera (Sumbawanga) na Juma Seph Kalambo.
Ruvuma ni Aden Nchimbi (Namtumbo), Gilbert Sinya (Mbinga), Ghaibu Lingo (Tunduru), Pendo Daniel (Songea) na Richard Mbambe (Nyasa).
Simiyu ni Albert Tuihwa (Bariadi), Rutaremwa Rutangumirwa (Maswa), Chele Ndaki (Meatu), Helman Tesha (Itilima) na Sebastian Masanja (Busega). Shinyanga ni Timonth Ndaya (Kaham), Shadrack Kengese () Kishapu) na Boniface Chambi (Shinyanga).
Singida ni Pius Songoma (Iramba), Deusdedith Duncun (Manyoni), Wilson Shimo (Singida), Flora Yongolo (Ikungi) na Omar Kipanga (Mkalama).
Songwe ni Johari Samizi (Songwe), Mary Marco (Ileje), Tusibetege Tengela (Mbozi) na Mathias Felix (Momba).
Tabora ni (Sweetbert Nkuba (Tabora), Moses Pesha (Uyui), Paschal Byemelwa (Urambo), Godslove Kawiche (Igunga), Onesmo Kisoka (Nzega), Renatus Mahimbali (Sikonge) na Jones Likuda (Kaliua).
Tanga ni Veronika Kinyemi (Lushoto), Mariagrace Kallega (Korogwe), John Mahali (Handeni), Faiza Salim (Tanga), Desderia Haule (Muheza), Ebene Mabuga (Pangani), Joseph Sura (Mkinga) na Philis Nyimbi (Kilindi).

Hakuna maoni: