Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya 
CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho 
kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu 
mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.
Kamati Kuu ni kikao kizito sana, 
hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao 
wanaosemekana kuwa wamehama chama, alisema mjumbe huyo.
Aliyekuwa
 Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono 
waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia 
yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) Machi 2010.
 
Mwigizaji
 Jackline Wolper akiongea katika mkutano wa Edward Lowassa aliofanya na 
Wanawake wa CHADEMA jiji Dar es Salaam Agosti 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni