ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 21 Julai 2016

Serikali kupaisha zaidi udahili vyuo vikuu



Imeandikwa na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema katika kutekeleza Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo (FYDP II) kwenye sekta ya elimu, imepanga kuleta mageuzi ya elimu kwa kuhakikisha inaongeza udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka asilimia 3.3 ya sasa hadi kufikia asilimia 6.9 ifikapo mwaka 2020.
Mkakati huo unalenga kuimarisha kiwango cha ubora wa elimu inayotolewa nchini ili kupata wahitimu wenye uwezo wa kuwajibika katika maeneo yao ya kazi na kutengeneza ajira, hivyo kuiwezesha Serikali kufikia lengo la Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Hatua hiyo, imetokana na ukweli kuwa pamoja na nchi kuwa na idadi kubwa ya watu inayoongezeka mwaka hadi mwaka, bado takwimu zinaonesha udahili wa wanafunzi katika vyuo vya elimu ya juu ni mdogo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara.
Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akifungua Maonesho ya 11 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
Alisema katika mwaka wa masomo 2015/2016 jumla ya wanafunzi 224,080 ndio waliodahiliwa, sawa na asilimia 3.3. Alisema kiwango hicho hakijafikia wastani wa chini uliowekwa na nchi za Jangwa la Sahara wa asilimia sita.
Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo sasa ni wakati wa Watanzania kuwekeza kwa nguvu zote katika elimu ili kuongeza fursa na usawa kama sharti la kufikia malengo ya taifa ifikapo mwaka 2025.
Alisema kupitia mpango huo, moja ya mageuzi katika mfumo wa elimu yanayotarajiwa pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi kujiunga na elimu ya juu ni kuhakikisha asilimia 56 ya wahitimu ifikapo mwaka 2020 ni wale waliobobea katika fani za sayansi na uhandisi.
Profesa Ndalichako alisema; “Ni kweli kuwa kwa sasa idadi ya vyuo na wanafunzi wanaodahiliwa imeongezeka kuliko miaka ya nyuma, lakini kitendo cha wanafunzi hao kupokea shahada pekee hakitoshi. Lazima vyuo hivi vihakikishe elimu wanayoitoa inawawezesha wahitimu hawa kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye.”
ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu
kuwa inaanza kutoa elimu ya pre-form one kwaajili ya maandalizi ya kidato cha kwanza. Kuanzia tarehe 09/09/2016.Kwa gharama ya shilingi elfu ishirini(20,000) tu kwa muda wa miezi mitatu(3), ambapo mwanafunzi atapewa vitu vifuatavyo:-
1) Tisheti yenye jina la kituo
2) Daftali, peni na pensel
3) Vitabu vya masomo husika yakiwemo biology, English,physic
4) Mitihani kila wiki kupima maendeleo ya mwanafunzi
Pia Kikoti education centre wanaendelea na kutoa tuition kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita kama kawaida
OUR MOTTO: EDUCATION FOR LIFE
Kwa mawasiliano zaidi tupigio kwa namba 0769694963

Hakuna maoni: