Jumanne, 31 Mei 2016
Jumatatu, 30 Mei 2016
Jumapili, 29 Mei 2016
Wanafunzi wamtuhumu Makamu Mkuu wa shule kulawiti
Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani.
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016.
Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.
Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.
Kufuatia msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi, Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza na wanafunzi hao.
Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria. “Msitaharuki mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote ile,” alisisitiza.
Wanafunzi 7,000 Watimuliwa UDOM
Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi
7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na
kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja.
Jana, lilitolewa
tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi
leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo
yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao
kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alipotakiwa kufafanua suala
hilo, alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe
simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.
Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la Serikali na wametakiwa kulitekeleza.
Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo watakapoelekezwa vinginevyo.
Hata
hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna
walivyopewa taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa
kuondoka.
Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa
maalumu kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la
walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.
Waliokuwa na
sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha
nne na kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)